Adhabu hiyo kali ilianza kutumika huko Uajemi na kuenea hadi Dola la Roma ambalo liliitumia hasa katika maeneo ya pembeni na kwa watumwa.
Kadiri ya Injili zote nne, Ponsyo Pilato, liwali wa Palestina (26-36), aliamua Yesu aadhibiwe hivyo kulingana na shtaka la viongozi wa Wayahudi waliodai kwamba mtuhumiwa alijitangaza kuwa mfalme na kupinga mamlaka ya Kaisari wa Roma, kwa wakati huo Tiberius, ingawa Pilato alikuwa ametambua shtaka halikuwa la kweli, bali lilitokana na husuda.
Kadiri ya Injili ya Yohane, Pilato mwenyewe alisisitiza kwamba, katika maandishi yaliyotakiwa kuwajulisha watu sababu ya adhabu hiyo, iwekwe wazi kwamba Yesu aliuawa kama mfalme wa Wayahudi, ingawa neno hilo lilichukiza viongozi wa taifa.
Maneno ya ilani hiyo yaliandikwa katika lughatatu:
Kilatini: Iesus Nazarenus Rex Iudeorum, kifupi INRI,
Kigiriki: Ἰησοῦς ὁ Ναζωραῖος ὁ Bασιλεὺς τῶν Ἰουδαίω. Kutokana na herufi hizo, Wagiriki wanaandika INBI.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Msalaba wa Yesu kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!