Mifano ya Yesu inaweza kusomwa katika Injili zote nne za Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo, lakini pia katika Injili nyingine zilizoandikwa baadaye. Injili ya Luka ndiyo inayoongoza kwa wingi wa mifano (50 hivi).
Wakristo wanatia maanani sana mifano hiyo kama maneno ya Yesu yanayohitaji kufikiriwa zaidi ili kuelewa yanataka kusema nini kweli.[1][2]
Ni kwamba mifano ya Yesu inaonekana kwanza hadithi za kuvutia zinazochora vizuri maisha ya watu yalivyokuwa katika mazingira yake. Hata hivyo wataalamu wanaonyesha kwamba ujumbe wa dhati umefichika hasa katika sehemu ya mwisho ya habari, ambapo kuna jambo lisilo la kawaida, yaani lisilotokea kweli.[3][4]
Ingawa mifano inaonekana kusimulia habari za kawaida, lengo ni kufikisha ujumbe wa kidini kwa wasikilizaji wenye nia njema, ambao wanapokea changamoto ya Yesu, "Mwenye masikio, na asikie!".
Mifano ya Yesu inabaki kati ya masimulizi maarufu zaidi duniani kote.[5]
Kwa Kiebranianeno husika ni מָשָׁל mashal linalodokeza pia fumbo au kitendawili. Agano la Kale lilikuwa tayari na mifano ya namna hiyo, hivyo Wayahudi wa wakati wa Yesu waliweza kuelewa ya kwake kwa urahisi fulani.[6]
Tanbihi
↑J. Dwight Pentecost, 1998 The parables of Jesus: lessons in life from the Master TeacherISBN 0-8254-3458-0 page 10
↑Eric Francis Osborn, 1993 The emergence of Christian theologyISBN 0-521-43078-X page 98
↑Friedrich Gustav Lisco 1850 The Parables of Jesus Daniels and Smith Publishers, Philadelphia pages 9–11
↑Ashton Oxenden, 1864 The parables of our Lord William Macintosh Publishers, London, page 6
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mifano ya Yesu kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!