Baada ya Aleksander Mkuu wasemaji wa Kiaramu walitawaliwa na watu wa ustaarabu wa Kigiriki. Katika miji mikubwa Kigiriki kilikuwa lugha kuu. Baada ya uenezaji wa Ukristo lugha hiyo iliendelea ikajulikana zaidi kama "Kisiria".
Hata baada ya uenezi wa Uislamu Kisiria kiliendelea kupanuka na vitabu vingi viliandikwa kwa lugha hiyo. Hata hivyo polepole wasemaji wengi wa Kisiria walianza kutumia Kiarabu, hasa wale waliogeukia Uislamu.
Pamoja na hayo watu 445,000 hivi wanaitumia hata leo, hasa nchini Syria, Iraq na Uturuki. Karibu wote ni Wakristo.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kiaramu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!