Nchi inatajwa pia kwa jina la "Shamu" katika maandiko ya Kiswahili, ingawa neno hili lamaanisha zaidi eneo la kihistoria ambalo lilikuwa kubwa kuliko Syria ya leo.
Historia
Nchi ilikaliwa na watu tangu milenia nyingi. Ilipata kuwa chini ya utawala wa Misri hadi mnamo mwaka 1100 KK.
Tangu mwaka 64 KKDola la Roma likaingia Shamu. Dameski ikawa mji mkuu wa jimbo la Kiroma likakua na kustawi. Barabara na majengo ya nyakati zile za Waroma yanaonekana hadi leo, kwa mfano barabara ya decumanus, ambayo imetajwa katika Biblia ya Kikristo kama "barabara iliyonyoka" au "barabara iitwayo Nyofu" (Mdo 9:11).
Wakati wa utawala wa Waosmani, Wayahudi na Wakristo wa Dameski waliweza kuendelea na dini zao wakiwa dhimmi (watu wasio Waislamu na waliolazimisha kulipa kodi kubwa kuliko ya Waislamu).
Mwaka 1925, mapinduzi mapya ambayo yalianzishwa na Hauran (eneo la mashambakusini mwa nchi) yalifika Dameski. Wasyria walitaka uhuru wao. Lakini, Ufaransa ulitupa mabomu Dameski na waliacha mapinduzi.
Syria ilishiriki katika vita vya Waarabu dhidi ya Israel. Hivyo sehemu ya Mkoa wa Qunaytrah imekaliwa na Israel tangu mwaka 1967.
Tangu Machi 2011 nchi imeingia vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoua watu zaidi ya 100,000 kufikia Septemba 2013 na kufanya wananchi milioni 9.5 kukimbia nyumba zao. Kati yao milioni 4 wako nje ya nchi. Wakati fulani nusu ya nchi ilitawaliwa na DAESH.
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Syria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.