Nchi

Ramani ya kitopografia ya Ulaya.
Ramani sawa na ya hapo juu, lakini ikionyesha mataifa huru ambayo yamekubaliwa na Umoja wa Mataifa badala ya topografia.

Nchi kwa maana ya msingi ni Dunia, hasa sehemu yake isiyofunikwa na bahari. Mara nyingi zaidi inataja sehemu maalumu iliyogawanyika kisiasa kwa mipaka na kutajawa kwa jina lake. Kwa maana hiyo ya kawaida nchi ni kitengo cha kisiasa katika eneo maalumu. Kwa kawaida nchi ni pia dola, lakini ziko pia nchi ambazo ni sehemu ya dola kubwa zaidi.

Katika baadhi ya matumizi inaashiria majimbo na vitengo vingine vya kisiasa[1][2][3] ilihali katika mengine inahusu tu majimbo [4]. Si nadra kwa taarifa ya ujumla au machapisho ya takwimu kuchukua ufafanuzi mpana wa neno hili kwa makusudi kama maonyesho na ulinganifu.[5][6][7][8][9]

Baadhi ya maeneo yaliyokuwa zamani nchi au pia madola ya pekee na baadaye sehemu za dola kubwa zaidi, bado zinajulikana kama "nchi" hasa kama yametunza kiasi cha utamaduni wao, kama vile Uingereza, Uskoti na Welisi - katika Ufalme wa Muungano.[10][11][12][13] Kihistoria, nchi za Umoja wa zamani wa Kisovyeti na Yugoslavia zilikuwa nyingine za namna hiyo. Majimbo ya zamani kama Bavaria (sasa ni sehemu ya Ujerumani) na Piemonte (sasa ni sehemu ya Italia) yangekuwa si kawaida kujulikana kama "nchi" katika Kiingereza cha kisasa.

Kiwango cha uhuru wa nchi zisizo mataifa inatofautiana sana. Baadhi ni mali ya mataifa, kwani mataifa kadhaa yana maeneo yanayoyategemea ya ng'ambo (kama vile Visiwa vya Virgin vya Uingereza, Saint Pierre na Miquelon, na Samoa ya Marekani), yenye eneo na raia tofauti na yao wenyewe. Maeneo tegemezi kama hayo wakati mwingine yanatajwa pamoja na mataifa huru kwenye orodha ya nchi, na yanaweza kuchukuliwa kama "nchi ya asili" katika biashara ya kimataifa, kama Hong Kong ilivyo. Baadhi ya nchi zimegawanywa kati ya madola kadhaa, kama vile Korea na Kurdistan.

Asili na maendeleo ya neno

Neno nchi kwa Kiingereza limetokana na neno la Kilatini contra, maana yake "dhidi", inayotumika katika maana ya "inayolalia, au kinyume na, mtazamo", yaani hali ya ardhi ilivyoenea nje kwa mtazamo. Kutoka hili likaja neno la Mwishoni mwa Kilatini contrata, ambalo lilikuja kuwa contrada ya Kiitalia ya kisasa. Neno hili linaonekana katika Kiingereza cha Enzi za Kati kutoka karne ya 13, tayari katika hisia mbalimbali.[14]

Maneno sawa katika lugha ya Kifaransa na lugha za Kirumi (pays na variants) hayajabeba mchakato wa kutambuliwa na majimbo ya kisiasa yaliyo huru kama "nchi" katika Kiingereza, na katika nchi nyingi za Ulaya maneno haya hutumiwa kwa vitengo vidogo vya maeneo ya kitaifa, kama katika Länder ya Kijerumani, vilevile kama neno lisilo rasmi kwa jimbo au taifa huru. Ufaransa ina "pays" nyingi sana ambazo zinatambuliwa rasmi katika kiwango fulani, na ni aidha kanda ya asili, kama Pays de Bray, au zinaashiria miungano ya kale ya kisiasa au kiuchumi, kama Pays de la Loire. Wakati huo huo Wales, Marekani, na Brazili pia ni "pays" katika matamshi ya kila siku Kifaransa.

Angalia pia

Marejeo

  1. "Acts Interpretation Act 1901 - Sect 22: Meaning of certain words". Australasian Legal Information Institute. Iliwekwa mnamo 2008-11-12.
  2. "The Kwet Koe v Minister for Immigration & Ethnic Affairs & Ors [1997] FCA 912 (8 September 1997)". Australasian Legal Information Institute. Iliwekwa mnamo 2008-11-12.
  3. "U.S. Department of State Foreign Affairs Manual Volume 2—General" (PDF). United States Department of State. Iliwekwa mnamo 2008-11-12.
  4. Rosenberg, Matt. "Geography: Country, State, and Nation". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-06. Iliwekwa mnamo 2008-11-12.
  5. "Greenland Country Information". Countryreports.org. Iliwekwa mnamo 2008-05-28. "The World Factbook - Rank Order - Exports". Central Intelligence Agency. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-10-04. Iliwekwa mnamo 2008-11-12.
  6. "Index of Economic Freedom". The Heritage Foundation. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-11-14. Iliwekwa mnamo 2008-11-12.
  7. "Index of Economic Freedom - Top 10 Countries". The Heritage Foundation. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-01-24. Iliwekwa mnamo 2008-11-12.
  8. "Asia-Pacific (Region A) Economic Information" (PDF). The Heritage Foundation. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2008-11-14. Iliwekwa mnamo 2008-11-12.
  9. "Subjective well-being in 97 countries" (PDF). University of Michigan. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2008-08-19. Iliwekwa mnamo 2008-11-12.
  10. "Legal Research Guide: United Kingdom - Law Library of Congress (Library of Cong". Library of Congress website. Library of Congress. 2009-07-23. Iliwekwa mnamo 2009-09-22. The United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland is the collective name of four countries, England, Wales, Scotland and Northern Ireland. The four separate countries were united under a single Parliament through a series of Acts of Union.
  11. "countries within a country:number10.gov.uk". 10 Downing Street website. 10 Downing Street. 2003-01-10. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-09-09. Iliwekwa mnamo 2009-09-22. The United Kingdom is made up of four countries: England, Scotland, Wales and Northern Ireland.
  12. "Commonwealth Secretariat - Geography". Commonwealth Secretariat website. Commonwealth Secretariat. 2009-09-22. Iliwekwa mnamo 2009-09-22. The United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland (UK) is a union of four countries: England, Scotland, Wales and Northern Ireland.
  13. "Travelling Europe - United Kingdom". European Youth Portal. European Commission. 2009-06-29. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-02-05. Iliwekwa mnamo 2009-09-22. The United Kingdom is made up of four countries: England, Northern Ireland, Scotland and Wales.
  14. John Simpson, Edmund Weiner, ed. "country". Oxford English Dictionary (1971 compact ed.). Oxford, England: Oxford University Press. ISBN 0198611862 .

Viungo vya nje

Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!