Mahali pa Uingereza (kijani cheusi) kwenye visiwa vya Britania ndani ya Ufalme wa Muungano (kijani nyeupe) pamoja na Jamhuri ya Eire (buluu) upande wa magharibi
Katika lugha ya kila siku "Uingereza" hutaja mara nyingi Ufalme wote au kisiwa chote cha Britania. Lakini kwa usahihi "Uingereza" ni ile sehemu kubwa zaidi kusini mwa kisiwa, tofauti na nchi za Welisi (Wales, upande wa magharibi) na Uskoti (Scotland, upande wa kaskazini).
Asili ya jina la Kiswahili ni neno إنجليزي injilisi(matamshi ya Kimisri: ingilisi)" katika lugha ya Kiarabu; Waarabu walisikia jina "inglish" wakirahisisha matamshi kuwa "inglis", wakaongeza sauti fupi kati ya "g" na "l", hivyo kufikia kwa "ingilis" ambako "i" ya pili ni fupi kiasi cha kusikia pia "e" na hivyo ilipokewa na Waswahili. Kwa namna ya Kibantu sauti ya "l" ikawa "r": ingelesi kuwa ingereza.
Jiografia
Uingereza iko kwenye kisiwa cha Britania ambacho ndicho kisiwa kikubwa cha Ulaya. Inapakana na Welisi upande wa magharibi na Uskoti upande wa kaskazini.
Uingereza ina visiwa vingi vidogo; kikubwa ni Isle of Wight katika kusini. Pwani zake ni ndefu, hakuna mahali palipo mbali zaidi ya km 113 kutoka baharini.
Sehemu kubwa ya nchi ni ama tambarare au vilima vidogo; mwinuko wa juu ni Scafell Pike yenye kimo cha mita 978. Kumbe milima mirefu ya Britania iko Welisi na Uskoti.
Tabianchi
Tabianchi ya Uingereza inaathiriwa na mahali pake baharini inayopitiwa na Mkondo wa Ghuba na latitudo ya kaskazini. Athari hizo zinaleta tabianchi fufutende ya kibahari; kwa wastanibaridi haishuki chini ya 0 °C na joto halipandi juu ya 32 °C. Hata hivyo vipindi vya jeledi au joto kali zaidi vinaweza kutokea kwa siku kadhaa. Miezi ya baridi ni Januari na Februari. Julai kwa kawaida ni mwezi wenye joto zaidi. Hali ya hewa mara nyingi ni nyevunyevu na mvua inaweza kutokea mwaka wote. Vipindi vya mvua na jua hubadilishana haraka.
Kihistoria Uingereza iligawiwa katika kaunti (counties) na miji (boroughs).
Nchi yote imegawiwa leo katika mikoa (regions) 9. Mikoa kadhaa huwa na mamlaka fulani ya kiutawala, lakini si yote. Vinginevyo utawala wa kieneo kunatokea hasa kwenye ngazi ya kaunti na halmashauri ndani ya kila mkoa.
Wabritania na Waroma waliokuwa wamebaki walihamia maeneo ya kando kama Welisi au Cornwall au kuvuka mfereji wa Uingereza kwenda Britania Ndogo (Kiingereza: Brittany; Kifaransa: Bretagne).
Mwaka 1066 wanajeshi Wanormani kutoka kaskazini mwa Ufaransa walivamia Uingereza na kuiteka yote chini ya mtemi William Mshindi. Wavamizi walitawala wakitumia aina ya Kifaransa. Lugha zote mbili za wananchi na za mabwana ziliendelea pamoja sambamba hadi kuwa lugha moja cha Kiingereza.
Ufalme wa Muungano
Tangu mwaka 1601 mfalme James VI wa Uskoti alichaguliwa kuwa mfalme wa Uingereza pia. Nchi jirani zote mbili ziliendelea na wafalme wa pamoja hadi mwaka 1707. Mwaka ule Uingereza pamoja na Welisi na Uskoti ziliunganishwa kuwa Ufalme wa Muungano wa Britania.