Karne ya 5 ilikuwa kipindi cha miaka mia moja kati ya 401 na 500. Kikamilifu kilianza tarehe 1 Januari 401 na kuishia 31 Desemba 600. Namba zake zinafuata hesabu ya miaka "baada ya Kristo".
Kama kila "karne" ni kipindi kinachohesabiwa kwa hiari ya binadamu kwa sababu ni mgawanyo wa kalenda tu: katika hali halisi maendeleo na mabadiliko makubwa hayafuati migawanyo ya kalenda ya kibinadamu.
Kuna mambo mengi yaliyotokea wakati wa karne hii, kama haya yafuatayo.
Matukio
Watu muhimu
- Agostino wa Hippo (354-430), askofu na babu wa Kanisa
- Alariko I, mfalme wa Wavisigoti aliyeteka Roma
- Ambrosi, askofu na babu wa Kanisa
- Atila, mfalme wa Wahuni
- Jeromu, padri na babu wa Kanisa
- Klovis, mfalme wa Wafaranki, wa kwanza kupokea Ukristo wa Kikatoliki
- Mesrop, mtakatifu aliyebuni alfabeti ya Kiarmenia (405 hivi)
- Papa Leo I, babu wa Kanisa
- Patrisi, askofu na mmisionari wa Ireland
- Theodoriko, mfalme wa Waostrogoti
- Yohane Krisostomo, askofu na babu wa Kanisa