Ndiye Papa wa kwanza kuitwa "Mkuu" kutokana na mchango mkubwa alioutoa si tu upande wa dini bali pia wa siasa akiwajibika kuhudumia taifa la Mungu kwa kila namna. Ni kati ya Mapapa bora waliolipatia Kanisa la Roma sifa na kuliimarishia mamlaka yake wakati ile ya serikali ya jiji hilo ilipokuwa inafifia zaidi na zaidi.
Akiwa huko, Papa Sixtus III alifariki (11 Agosti440), na Leo alichaguliwa na umati kwa kauli moja kushika nafasi yake.
Papa
Tarehe 29 Septemba alianza kazi yake kama Papa ambayo ilichangia sana kukusanya mamlaka ya Kanisa lote katika jimbo la Roma, aliloliunda upya pamoja na majimbo mengine ya Italia.
Ili kuimarisha nafasi hiyo ya Kanisa pekee la Magharibi lililoanzishwa na mitume, alijitafutia hati maalumu kwa Kaisari Valentiniano II. Hiyo haikupendeza Wakristo wa Mashariki.
Nafasi bora ya kusisitiza kwa busara mamlaka hiyo hata upande wa mashariki ilitolewa na mabishano kuhusu nafsi ya Yesu Kristo yaliyosababishwa na Eutike kukanusha ubinadamu halisi wa Kristo.
Hata hivyo mwaka huohuo mtaguso unaojulikana kama Wizi wa Efeso ulipuuzia waraka huo usisomwe, ukamtetea Eutike. Hapo Leo akashika uongozi wa mapambano dhidi yake.
Mwaka 451 katika Mtaguso wa Kalsedonia, baada ya barua yake kwa Flavianus kusomwa, maaskofu wote 350 walisimama na kulia: "Ndiyo imani ya mababu... Mtume Petro amesema kwa njia ya Leo..." Hivyo ilithibitishwa imani katika hali mbili za Kristo zisizochanganyikana wala kutenganika.
Hata hivyo mabalozi wa Leo hawakuwekwa kati ya viongozi wa mtaguso, na kanuni ya 28 ilidai Kanisa la Konstantinopoli kuwa muhimu sawa na la Roma. Kwa hiyo Leo aliikataa, akisisitiza nafasi ya kwanza ya Roma ili kudumisha umoja hasa katika kipindi hicho cha fujo.
Vilevile, Leo alipambana kwa nguvu na Wapelaji, Wamani na Waprishila akitetea daima imani kadiri ya mapokeo ya mitume, akiunganisha vizuri ajabu unyenyekevu wake mwenyewe na hakika juu ya ukuu wa cheo chake kama mwandamizi wa Mtume Petro; vilevile alipambana na ushirikina wa Wapagani.
Siasa
Wakati Dola la Roma lilipokuwa likisambaratika, Leo alipata umaarufu pia kwa kutumia mamlaka yake ya kiroho tu ili kuzuia uvamizi wa Roma uliohofiwa kufanywa na Atila, mfalme wa Wauni (452) na ili kupunguza madhara ya ule uliofanywa na Wavandali kwa wiki mbili (455). Tena alistawisha matendo ya huruma mjini kwa waliopatwa na njaa, dhuluma na ufukara, kama vile umati wa wakimbizi.
Umuhimu wa Upapa wa Leo, ambao ulidumu muda mrefu kuliko Mapapa karibu wote, ni katika kusisitiza hata kwa madondoo ya Biblia mamlaka ya pekee ambayo Kanisa la Roma linayo juu ya makanisa yote duniani kutokana na Mtume Petro kuwekwa na Kristo na kufia Roma walipo waandamizi wake.
Ndilo fundisho linalojitokeza mfululizo katika barua zake 143 na hasa katika hotuba 96 zilizopo hata leo.
Humo unajitokeza utajiri na uwazi wa mafundisho aliyoyatoa kwa lugha sahili na safi. Ndio mkusanyo wa kwanza wa hotuba za Kipapa zilizochangia sana ustawi wa Kanisa baadaye.
Aliunganisha matendo ya ibada na maisha ya kila siku ya Wakristo, k.mf. saumu na matendo ya huruma. Alionyesha kuwa liturujia ya Kikristo si kumbukumbu ya matukio yaliyopita, bali utimiaji wa mambo yasiyoonekana katika maisha ya kila mmoja. Hivyo ni lazima Pasaka iadhimishwe kila wakati wa mwaka, “si kama jambo la zamani, bali kama tukio la leo”. Hata siku hizi Liturujia ya Roma inazidi kutumia matini yake mengi na kufuata mtindo wake bora katika sala.
↑Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
Vyanzo
Louise Ropes Loomis, The Book of Popes(Liber Pontificalis). Merchantville, NJ: Evolution Publishing. ISBN 1-889758-86-8 (Reprint of the 1916 edition. English translation with scholarly footnotes, and illustrations).
T. Jalland, The Life and Times of St. Leo the Great, (London, 1941).