Roma ina wakazi 2,860,009 katika 1,285 km2 (496.1 sq mi),[1] Roma ni komune yenye watu wengi zaidi nchini na ni jiji la tatu lenye watu wengi katika Umoja wa Ulaya kwa idadi ya watu ndani ya mipaka ya jiji.
Roma mara nyingi inajulikana kama Jiji la Milima Saba kutokana na eneo lake la kijiografia, na pia kama "Mji wa Milele". Roma kwa ujumla inachukuliwa kuwa "chimbuko la ustaarabu wa magharibi na Utamaduni wa Kikristo", na kitovu cha Kanisa Katoliki.[2][3][4]Mji wa Vatikano[5] (nchi ndogo zaidi duniani) ni nchi huru ndani ya mipaka ya jiji la Roma, mfano pekee uliopo wa nchi ndani ya jiji.
Tangu kuondoka kwa makao makuu ya Kaisari na kupungua kwa nguvu ya Dola la Roma Magharibiidadi ya wakazi ilipungua hadi kuwa na takriban 100,000 mnamo mwaka 530.
Katika karne zilizofuata Italia pamoja na Ulaya iliona vita na mashambulio ya makabila yasiyostaarabika. Mnamo mwaka 1000 Roma ilikuwa mji mdogo wenye wakazi 20,000 pekee walioishi ndani ya maghofu ya mji mkubwa wa kale.
Tangu kuimarika kwa utawala wa mapapa mji ulianza kukua tena; mnamo mwaka 1900 ukawa na wakazi 400,000. Katika karne ya 20 mji ulipanuka sana hadi kufikia idadi ya wakazi wa zamani hata kuipita. Siku hizi asilimia 7.4 ni wageni.
Orodha inayofuata inaonyesha makadirio hadi 1858, baadaye ni namba za sensa.
Roma ndiyo kitovu kimojawapo cha sekta ya viwanda na sekta ya huduma ya Italia. Utalii ni pia muhimu sana kiuchumi, kutokana na watalii 26,100,000 wanaoutembelea kila mwaka: 6.5% za Jumla ya Pato la Taifa zinapatikana ndani ya Roma ambazo ni kushinda miji mingine yote ya Italia.
Info-RomaIlihifadhiwa 23 Machi 2018 kwenye Wayback Machine. - Info-Rome ni tovuti kuhusu mambo ya kitalii katika mji wa Roma, hasa matukio ya aina mbalimbali, hoteli, maonyesho, nyumba za kumbukumbu na vyakula.
Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Roma kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!