Zimehesabiwa hadi lugha 23 za namna hiyo, ingawa baadhi kwa wengine ni lahaja tu. Tena kuna Krioli nyingi zenye asili katika lugha hizo. Kati ya Krioli hizo, ile ya Haiti na ile ya Shelisheli ni lugha rasmi nchini.
Kilatini kiliendelea kuwa lugha ya watu wengi katika maeneo mbalimbali ya himaya hii kubwa hasa mijini.
Katika sehemu hizo zilijitokeza lahaja za pekee kulingana na lugha asilia za wenyeji.
Baada ya kuporomoka kwa Dola la Roma la Magharibi, lahaja hizo za Kilatini katika nchi mbalimbali ziliendelea kuchanganyikana na lugha hizo na zile za makabila ya Wagermanik yaliyoteka maeneo hayo yote na hatimaye zikawa lugha za pekee.
Lugha za Kirumi zinazotumiwa kitaifa:
Lugha ambazo ni muhimi zaidi kama lugha za kitaifa ni:
Kirumanj (Rumantsch/Romontsch/Rumauntsch) (Jimbo la Graubünden, Uswisi) - wasemaji 27,000
Lugha za kimataifa
Lugha za Kihispania, Kifaransa na Kireno zimesambaa duniani kwa sababu ni lugha kuu za nchi ambazo zilikuwa na makoloni mengi, zikaacha lugha zao katika nchi nyingi, hasa Kihispania ambacho ni lugha kuu ya bara la Amerika, Kireno ambacho ni lugha rasmi ya Brazili na nchi 5 za Afrika na Kifaransa ambacho ni lugha rasmi katika nchi nyingi za Afrika, Amerika visiwani na Kanada.
Kiitalia ni mojawapo ya lugha rasmi za Uswisi, pamoja na nchi ndogondogo za San Marino na Vatikani.
Kiromania ni lugha rasmi ya Moldova pia, ingawa kwa jina la lahaja yake ya Kimoldova.
Tanbihi
Harris, Martin; Vincent, Nigel (1988). The Romance Languages. London: Routledge.
Posner, Rebecca (1996). The Romance Languages. Cambridge: Cambridge University Press.
Kibler, William W. (1984). An introduction to Old French. New York: Modern Language Association of America.
Kireno
Williams, Edwin B. (1968). From Latin to Portuguese, Historical Phonology and Morphology of the Portuguese Language (tol. la 2nd). University of Pennsylvania.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lugha za Kirumi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!