San Marino

San Marino


Mtazamo kutoka San Marino hadi bahari ya Adria.

San Marino (kwa Kiitalia maana yake ni "Mtakatifu Marino") ni kati ya nchi ndogo kabisa duniani. Eneo lake lote limo ndani ya mipaka ya Italia, kati ya wilaya za Rimini na Pesaro-Urbino, karibu na mwambao wa bahari ya Adria.

Eneo lote la km² 61,19 ni la milima.

Historia

San Marino inatajwa kuwa jamhuri yenye umri mkubwa kuliko zote duniani. Ilianzishwa na Wakristo waliokimbia dhuluma ya Kaisari wa Roma Diokletiano wakitafuta kimbilio mlimani.

Kati yao, shemasi Marino na padri Leo ndio maarufu zaidi.

Tangu hapo imefaulu kudumisha uhuru wake. Ndiyo sababu tangu mwaka 2008 imeorodheshwa na UNESCO kati ya mahali pa Urithi wa Dunia.

Watu

San Marino ina wakazi 33,909 (2019) katika vijiji 9. Karibu wote (97.2%) ni waumini wa Kanisa Katoliki (jimbo la San Marino-Montefeltro) na wanaongea Kiitalia kwa lahaja ya Kiromagna.

Siasa

San Marino imetunza utaratibu wa serikali inayofanana na muundo wa jamhuri ya Roma ya kale. Serikali inaongozwa na watawala wawili ("Capitani Reggenti") wanaochaguliwa kwa muda wa miezi sita tu kama zamani konsuli wa Kiroma.

Bunge linaitwa Halmashauri Kuu ("Consiglio Grande e Generale") likichaguliwa kila baada ya miaka mitano. Halmashauri inateua pia kamati ya watu 12 ("Consiglio dei XII") inayotekeleza kazi ya mahakama.

Wananchi wote hukutana mara mbili kwa mwaka kama mkutano mkubwa wa "Arengo" wakiamua juu ya matamko na mapendekezo kwa serikali.

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu San Marino kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!