Nchi ina wakazi milionitanounusu tu katika eneo la km² 338,000; hivyo ni kati ya nchi za Ulaya zenye msongamano mdogo wa watu. Sehemu kubwa ya eneo lake ni misitu tu. Mji mkuu ni Helsinki; mji muhimu mwingine ni Tampere, mji ulioko karibu kilomita 180 kaskazini mwa Helsinki, ni wa pili kwa ukubwa. Miji mingine mikubwa ni pamoja na Turku, Kuopio na Vaasa.
Waswidi wako hasa upande wa kusini mwa nchi, kwa jumla ni takriban 5% ya wakazi; hasa visiwa vya Aland kuna Waswidi watupu walio na hali ya kujitawala ndani ya Ufini.
Wakazi asilia ni Wasami ambao wako kaskazini tu. Maisha yao yanategemea uwindaji na ufugaji; wako wachache, jumla yao haifikii 0.2% ya wakazi wote.
Wakazi wenye lugha ya Kiswidi wako upande wa kusini mwa nchi kwa sababu Ufini ilitawaliwa na Uswidi kwa karne nyingi. Katika karne hizo walikuwepo Waswidi waliohamia Ufini lakini kuna pia Wafini walioanza kutumia Kiswidi pekee. Hasa kwenye visiwa vya Aland Kiswidi ni lugha pekee. Lakini Waswidi wa Ufini wanajisikia wa Ufini.
Upande wa dini, 72% ni Walutheri na 1.1% Waorthodoksi. Madhehebu hayo mawili ya Ukristo yanatambulika na kupewa nafasi katika matukio mbalimbali na shuleni. 1,6% wanafuata dini au madhehebu mengine, wakati 25.3% hawana dini yoyote.
↑Georg Haggren, Petri Halinen, Mika Lavento, Sami Raninen and Anna Wessman (2015). Muinaisuutemme jäljet. Helsinki: Gaudeamus. uk. 23. ISBN978-952-495-363-4.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
↑Georg Haggren, Petri Halinen, Mika Lavento, Sami Raninen ja Anna Wessman (2015). Muinaisuutemme jäljet. Helsinki: Gaudeamus. uk. 339. ISBN9789524953634.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
↑Finland was the first nation in the world to give all (adult) citizens full suffrage, in other words the right to vote and to run for office, in 1906. New Zealand was the first country in the world to grant all (adult) citizens the right to vote, in 1893. But women did not get the right to run for the New Zealand legislature, until 1919.
↑"Finland". International Monetary Fund. Iliwekwa mnamo 17 Aprili 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
↑"Fragile States Index 2016". Fundforpeace.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Februari 2017. Iliwekwa mnamo 27 Novemba 2016. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ufini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.