Asili ya jina ilikuwa nchi ya Wafilisti iliyokuwa kanda nyembamba ya ardhi karibu na pwani ya bahari. Waroma wa kale walitumia jina hilo kwa jumla ya jimbo lao katika sehemu hizi.
Baada ya uvamizi wa WaarabuWaislamu jina liliendelea kutumiwa kwa umbo la Kiarabu "Filastin" na kutazamwa kama sehemu ya Shamu au Syria.
Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya DuniaUingereza ulitawala eneo hili kama eneo la kukabidhiwa la Shirikisho la Mataifa, na eneo hili lilikuwa pamoja na sehemu kubwa upande wa mashariki wa mto Yordani. Waingereza waligawa eneo katika sehemu mbili upande wa magharibi (Palestina yenyewe) na upande wa mashariki wa mto Yordani uliokuwa baadaye milki ya Yordani.
Mwaka 1947Umoja wa Mataifa uliamua kugawa Palestina katika sehemu tatu zilizopangwa kama Dola la Kiyahudi, Dola la Kiarabu na Yerusalemu kama mji wa kimataifa. Lakini Wayahudi walitangaza uhuru wa Dola la Israeli. Wenyeji Waarabu walipinga azimio hili na vita ilitokea. Baada ya mkataba wa kusalimisha amri Israeli mpya ilikuwa na sehemu ya Palestina kubwa kuliko awali. Asilimia kubwa ya wakazi Waarabu wa sehemu zilizokuwa chini ya Israeli mpya walikimbia au walifukuzwa nje. Ukanda wa Gaza ulishikwa na Misri na Ukingo wa Magharibi wa Yordani ulitawaliwa na milki ya Yordani.
Kati ya wakimbizi Waarabu waliokaa katika makambi huko Lebanoni, Syria, Yordani na Gaza kulikuwa na harakati ya kujielewa kama taifa la Wapalestina wakaunda vyama mbalimbali vya kupigania kurudi kwao lakini hii ilishindikana. Baada ya Vita ya siku 6 mwaka 1967 Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Yordani zilitwaliwa na jeshi la Israeli.
Harakati ya Wapalestina Waarabu iliendelea kupigania uhuru. Mapigano haya yalipata namna ya usuluhisho kwa muda na katika mapatano ya Oslo mwaka 1993 yalianzishwa Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina yaliyotangaza Dola la Palestina.
Palestina mpya
Kwa sasa Palestina ni nchi katika mwendo wa kupata uhuru kamili lakini hakuna uhakika mwendo huu utakamilishwa lini.
Maeneo ya Palestina yanatengwa kati ya sehemu chini ya serikali ya Palestina na maeneo yanayosimamiwa na Israeli.
Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina ina kiwango fulani cha madaraka ya kiserikali katika baadhi ya maeneo haya.
Mamlaka hayo hutambuliwa na nchi nyingi za Waarabu kama serikali halisi. Jumuia ya kimataifa kwa ujumla imetambua mamlaka kwa viwango mbalimbali lakini si kama serikali kamili ya nchi huru. Hivyo Mamlaka ina kiti cha mtazamaji kwenye Umoja wa Mataifa.
1 Mapendekezo ya 1916-22 : Mapendekezo matatu kwa utawala wa Palestina baada ya Vita Kuu ya Kwanza. Mstari mwekundi ni mpaka wa "International Administration" iliyopendekezwa katika Mapatano ya Sykes–Picot ya 1916, mstari buluu uliokatwa ni pendekezo la 1919 la Shirika la Uzayuni kwenye Mkutano wa Paris 1919, Na mstari buluu mwembamba ni mipaka ya eneo la kukabidhiwa la Palestina chini ya mamlaka ya Uingereza 1923-48
2 Ardhi ya Kiyahudi 1947 : Ardhi iliyokuwa mali ya Wayahudi katika Eneo la kukabidhiwa la Palestina mnamo mwaka 1947. Idadi ya wakazi Wayahudi iliongezeka kuanzia watu 83,790 mwaka 1922 hadi 608,000 mwaka 1946.
3Mpango wa Umoja wa Kimataifa kwa Ugawaji wa Palestina 1947 : Azimio la UM lilitaka kugawa Palestina kwa sehemu tatu: Dola la Kiyahudi (nyeupe), Dola la Kiarabu (Kijani) na Yerusalemu kama mji wa pekee.
4 1948-67 : Baada ya vita ya uhuru wa Israel Ukanda wa Gaza ulibaki chini ya Misri na Ukingo wa Magharibi ya Yordani chini ya milki ya Yordani. Yerusalemu iligawiwa kati ya Israel na Yordani.
5 1993 hadi sasa: Maeneo yaliyo chini ya Serikali ya Palestina.
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Palestina kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!