Istanbul (kwa Kituruki unatajwa İstanbul) ni mji mkubwa zaidi katika nchi ya Uturuki, ukiwa na wakazi wanaokadiriwa kuwa kati ya milioni 11 na 15, ambao wanaufanya kuwa miongoni mwa miji mikubwa ya dunia. Huu ndio mji mkuu wa Mkoa wa İstanbul.
Eneo la Istanbul linaelekea pande zote mbili za mlangobahari wa Bosporus unaotenganisha Ulaya na Asia. Hivyo ni mji pekee duniani uliopo katika mabara mawili.
Wakati wa Waosmani majina mbalimbali yalitumiwa: Konstantinopoli au kwa kifupi "Konstantiniye", halafu tangu karne ya 18 pia "Istanbul". Tangu mwaka 1873jina rasmi kwa Kituruki limekuwa "Istanbul".
Hadi vita vya kwanza vya dunia Istanbul ilikuwa na wakazi wengi Wakristo, hasa Wagiriki na Waarmenia, lakini wakati ule Waarmenia waliteswa wakapungua na baada ya vita Wakristo walibaguliwa kwa jumla, hivyo wengi walihamia Ugiriki. Leo hii Wagiriki waliobaki ni 2000 - 3000 pekee na Waarmenia ni takriban 50,000.
Majengo
Istanbul huwa na majengo mengi ya kihistoria kama vile
Topkapi iliyokuwa ikulu ya masultani hadi mwaka 1923 na leo hii ni kati ya makumbusho muhimu duniani
Mnara wa Msichana - Kiz Kulesi: kulingana na hadithi nyingi tofauti, Konstantino, mmoja wa viongozi wa Kibizanti, alikuwa na binti yake mrembo ambaye alimpenda sana. Watabiri walitabiri kuwa kifo cha binti huyo kitatokana na kugongwa na nyoka. Katika kumlinda binti yake na janga hilo, mfalme akaagiza kujengwe nyumba katikati ya kisiwa ambapo ndipo Kiz Kulesi ilipo hivi sasa. Lakini mwisho wa siku yule binti aliuawa na nyoka aliyefika kisiwani katika kikapu cha mboga.
Elimu
Mjini Istanbul kuna vyuo vikuu mbalimbali, kati yake:
Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Istanbul kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.