Wakristo, wakiguswa na upendo wake, wanakubali changamoto ya kumfuata kwa kujitoa moja kwa moja kwa ajili ya watu wote.
Mbali na wafuasi wake, ambao wa kwanza walitokea dini ya Uyahudi, wana wa Israeli walimkataa moja kwa moja. Wataalamu wa Tanakh (Biblia ya Kiebrania) hawaoni utabiri wa manabii wa kale kutimia ndani mwake.
Katika Uislamu, Yesu (akiitwa kwa heshima nabii Isa bin Mariamu) ni kati ya manabii wakuu na wanaopendwa zaidi, lakini ni mtu tu, asiyetakiwa kabisa kulinganishwa na Mungu.
Dini ya Bahai inamtambua Yesu kama tokeo mojawapo la Mungu pekee, ambaye pamoja na wengine waliwaonyesha watu sifa za Mungu. Bahá'í inakanusha uwezekano wa Umungu kuwemo katika mwili wa mtu fulani tu.
Ubuddha na dini nyingine, hasa za Asia Mashariki, hazina mtazamo maalumu juu ya Yesu, kwa sababu zilianzishwa kabla ya ujio wake.
Watu wasio na dini wanamuona Yesu kama mtu wa kawaida, hata kama aliathiri sana historia ya dunia, au kama shujaa wa upendo aliyefundisha na kutekeleza maadili ya hali ya juu.
↑The Christology of Anselm of Canterbury by Dániel Deme 2004 ISBN 0-7546-3779-4 pages 199-200
↑The Christology of the New Testament by Oscar Cullmann 1959 ISBN 0-664-24351-7 page 79
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mitazamo juu ya Yesu kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!