Ujio wa pili

Picha takatifu ya Kigiriki ya ujio wa pili, 1700 hivi.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Yesu
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho  • Utoto wa Yesu  • Ubatizo
Arusi ya Kana • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu  • Miujiza ya Yesu
Kugeuka sura • Karamu ya mwisho • Msalaba wa Yesu  • Maneno saba
Kifo cha Yesu  • Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni  • Ujio wa pili
Injili  • Majina ya Yesu katika Agano Jipya  • Yesu kadiri ya historia  • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Ndugu wa Yesu • Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa

Hukumu ya mwisho ilivyochorwa na Michelangelo (1541).

Ujio wa pili ni imani ya kwamba Yesu, aliyekuja mara ya kwanza kwa unyenyekevu alipozaliwa na Bikira Maria, atashuka tena toka mbinguni kwa utukufu siku ya kiyama.

Katika Ukristo

Msingi wa tumaini hilo katika Ukristo ni ahadi alizotoa mwenyewe na ambazo zinasomwa katika Injili (Math 24:27; 25:31; Lk 17:30; Yoh 6:39-40).

Ufafanuzi zaidi ulitolewa na Mtume Paulo (Mdo 10:42; 17:31; Rom 2:5-16; 14:10; 1Kor 4:5; 15:23; 2Kor 5:10; Fil 1:6; 1Tim 6:14; 2 Tim 4:1,8; Tito 2:13; 1Thes 5:2; 2Thes 1:5; 2:1-9) na wengineo katika vitabu vingine vya Agano Jipya (1Pet 4:13; Yak 5:7) na baadaye.

Katika Agano Jipya neno ἐπιφάνεια, epiphaneia, kutokea, limetumika mara 5 kuhusiana na kurudi kwa Kristo,[1] kumbe neno παρουσία, parousia, kufika au kuwepo, mara 17.[2][3]

Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli (karne ya 4) ilikiri kwamba "atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu wazima na wafu, na ufalme wake hautakuwa na mwisho".

Hata hivyo Wakristo wanatofautiana kuhusu jambo hilo kadiri ya madhehebu yao, lakini pia kadiri ya rai binafsi kuhusu maana halisi ya maneno yake.

Kama Yesu mwenyewe alivyotabiri, jambo hilo litaleta udanganyifu mwingi ambao alitaka wafuasi wake wajihadari usiwapate.

Kweli karne hata karne walitokea watu kutabiri mwaka au hata tarehe ya tukio hilo; tena wengine walisema limeshafanyika, kumbe bado.

Yesu alisema, "Hakuna anayejua siku wala saa". Lakini watu hao walijaribu kutumia namba za Biblia ili kuhesabu itakuwa lini.

Katika Uislamu

Katika Islam, عيسى (ʿĪsā, Isa) anaheshimiwa kama mtume na Masihi aliyetumwa kwa Waisraeli (banī isrā'īl) akiwaletea kitabu kipya, Injili.[4]

Quran inazungumzia ujio wa pili wa huyo Yesu katika sura Az-zukhruf (43:61) kama ishara ya siku ya hukumu.[5][6]

Pia kuna Hadithi za Mtume Muhammad zinazotabiri wazi ujio wake.[7][8]

Tanbihi

  1. NT usage
  2. "Strong's G3952". Blueletterbible.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-10. Iliwekwa mnamo 2009-11-21.
  3. "CATHOLIC ENCYCLOPEDIA: General Judgment (Last Judgment)". Newadvent.org. 1910-10-01. Iliwekwa mnamo 2009-11-21.
  4. The Oxford Dictionary of Islam, p.158
  5. Yusuf Ali, Abdullah. "Surah Az-zukhruf". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-01-15. Iliwekwa mnamo 2014-09-02.
  6. kathir, Ibn. "Tafsir al-Qur'an al-Azim".
  7. "Isa", Encyclopedia of Islam
  8. Sonn (2004) p. 209

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ujio wa pili kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!