Pia zinasisitiza kwamba Yesu ni Mwana wa Daudi, yaani kwa njia ya Yosefu, ambaye kinasaba anatokana na mfalme huyo maarufu wa Agano la Kale, ana haki ya kurithi cheo chake.
Hata hivyo majina mengi ni tofauti katika orodha hizo mbili, kiasi kwamba wataalamu wanatoa maelezo mbalimbali kuhusiana na desturi za Israeli wakati ule, kwa mfano katika kutumia orodha ya vizazi, na kutokana na malengo ya Wainjili hao[1][2], ambao wote wawili walitaka kusisitiza kihisabati kwamba Yesu amefika kwa wakati mwafaka uliopangwa na Mungu kwa makini (vizazi 14x3 kadiri ya Mathayo; 7x11 kadiri ya Luka).
Akiwaandikia Wayahudi, mwinjili Mathayo alitaka kusisitiza kwamba Yesu ni Daudi mpya, lakini pia mrithi wa Abrahamu katika kuwa baraka kwa mataifa yote.
Akiwaandikia watu wa mataifa, mwinjili Luka alitaka kuonyesha kwamba Yesu ni mwana wa Adamu, hivyo anahusiana na binadamu wote.
Tanbihi
↑Marcus J. Borg, John Dominic Crossan, The First Christmas (HarperCollins, 2009) page 95.
↑R. T. France, The Gospel According to Matthew: An Introduction and Commentary (Eerdmans, 1985) page 71.
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ukoo wa Yesu kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!