Mathayo anakazia kuwa Yesu wa Nazareti ndiye Masiya aliyetangazwa na manabii wa Agano la Kale. Kwa sababu hiyo Mathayo anaripoti maneno ya Agano la Kale mara kwa mara ili kuthibitishwa yametimia katika maisha ya Yesu.
Tabia hii inachukuliwa kuthibitisha maelezo ya kwamba Injili hii ililenga Wakristo ambao walikuwa Wayahudi na kutumia lugha ya Kigiriki.
Mathayo anakazia pia mafundisho ya Yesu ilhali Marko anaeleza zaidi matendo yake.
Nembo ya Injili
Injili hii inaanza kwa kuorodhesha mababu wa Yesu. Kutokana na mwanzo huu, vizazi vya baadaye vilimpa Mwinjili Mathayo nembo la mwanamume au malaika akichora habari za Biblia.
Chanzo cha kazi yake huko Galilaya (Mat 3-4) Yohane Mbatizaji, Yesu ajaribiwa jangwani, Mitume wa kwanza
Hotuba ya mlimani (Mat 5-7)
Uponyaji na miujiza (Mat 8 – 9,34)
Hotuba kuhusu umisionari wa wanafunzi Wito wa mitume 12 (10,1-4), tangazo la mateso yajayo (10,16-26), hofu ya watu na kumhofia Mungu (10,26-33)
Mafundisho juu ya Yohane Mbatizaji, Wafarisayo na walimu wa sheria
Hotuba ya mifano juu ya Ufalme wa Mungu (Mat 13) Mfano wa mpanzi (13,1-9; maelezo 13,18-23), magugu katika ngano (13,24-30; maelezo 13,36-43), mfano wa mbegu wa haradali (13,31-32), chachu (13,33-35), hazina iliyofichika (13,44), lulu (13,45-46), wavu wa samaki (13,47-52)
Matendo mengine (Mat 13,53 - 17,27)
Hotuba juu ya mahusiano kati ya wanafunzi (Mat 18)
Safari ya kwenda Yerusalemu (Mat 19-22)
Hotuba juu ya mwisho wa Yerusalemu na mwisho wa nyakati (Mat 23-25)
Beaton, Richard C. (2005). "How Matthew Writes". Katika Bockmuehl, Markus; Hagner, Donald A. (whr.). The Written Gospel. Oxford University Press. ISBN978-0-521-83285-4. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
Wallace, Daniel B., mhr. (2011). Revisiting the Corruption of the New Testament: Manuscript, Patristic, and Apocryphal Evidence. Text and canon of the New Testament. Kregel Academic. ISBN9780825489068. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
Makala hii kuhusu mambo ya Agano Jipya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Injili ya Mathayo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.