Kwa kawaida wataalamu wa Biblia wanakadiria kwamba mwaka wa kubatizwa ulikuwa kati ya 27 na 29BK na ule wa kuuawa kati ya 30 na 33.[3]
Awali Yesu, baada ya kubatizwa na kukaa siku 40 katika jangwa la Yudea, alifanya kazi ya kitume zaidi katika mkoa wa Galilaya, huko alikokulia,[4] akihubiri na kuponya, pamoja na kufukuza pepo wachafu.
Mbali ya hiyo miujiza yake, ni muhimu mwenendo wake wa kukaribiana na watu wa kila aina, bila ubaguzi: tendo lake la kushiriki karamu pamoja na wakosefu lilichukiza wengi, hasa kati ya madhehebu ya Mafarisayo waliokwepa watu hao. Kumbe kwa Yesu lilikuwa dokezo la kwamba Mungu anawaalika wote kutubu na kuingia raha ya ufalme wake.
Mtume Petro alisimulia kifupi utume wa Yesu kama ifuatavyo (Mdo 10:34-43):
34 Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo; 35 bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye. 36 Neno lile alilowapelekea wana wa Israeli akihubiri habari njema ya amani kwa Yesu Kristo (ndiye Bwana wa wote), 37 jambo lile ninyi mmelijua, lililoenea katika Uyahudi wote likianzia Galilaya, baada ya ubatizo aliouhubiri Yohana; 38 habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye. 39 Nasi tu mashahidi wa mambo yote aliyoyatenda katika nchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu; ambaye walimwua wakamtundika mtini. 40 Huyo Mungu alimfufua siku ya tatu, akamjalia kudhihirika, 41 si kwa watu wote, bali kwa mashahidi waliokuwa wamekwisha kuchaguliwa na Mungu, ndio sisi, tuliokula na kunywa pamoja naye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu. 42 Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudia ya kuwa huyu ndiye aliyeamriwa na Mungu awe Mhukumu wa walio hai na wafu. 43 Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi.
↑Paul L. Maier "The Date of the Nativity and Chronology of Jesus" in Chronos, kairos, Christos: nativity and chronological studies by Jerry Vardaman, Edwin M. Yamauchi 1989 ISBN 0-931464-50-1 pages 113-129
↑Jesus & the Rise of Early Christianity: A History of New Testament Times by Paul Barnett 2002 ISBN 0-8308-2699-8 pages 19-21
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Utume wa Yesu kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!