Mitazamo ya Kiyahudi juu ya Yesu ni ya aina mbalimbali, lakini yote haimkubali, la sivyo ingewabidi wahusika wamuamini na kubatizwa badala ya kuendelea na dini yao ambayo viongozi wake walimhukumu ni kafiri anayestahili kuuawa.
Kwa kawaida Wayahudi wanamuona Yesu kama mmojawapo kati ya wengi waliojinadi kuwa Masiya katika nyakati mbalimbali za historia ya taifa lao.[1]
Yesu anatazamwa kama yule aliyefaulu zaidi kukubalika, na kwa sababu hiyo, kuleta madhara makubwa kuliko wote.[2]
Uyahudi haujawahi kumkubali rasmi Masiya yeyote kuwa ametimiza utabiri wa manabii. Zaidi ya hayo, unaona ibada ya Wakristo kwa Yesu kuwa kinyume cha imani katika Mungu mmoja tu.[3]
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mitazamo ya Kiyahudi juu ya Yesu kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.