Malkia wa Mbingu (kwa Kilatini: Regina caeli; tamka: reˈdʒina ˈtʃeli) ni sifa mojawapo ya Bikira Maria katika Kanisa la Kilatini inayotumika hasa katika sala maalumu ya wakati wa Pasaka, kuanzia Dominika ya Ufufuko wa Yesu hadi Pentekoste.
Katika siku hizo hamsini Malkia wa Mbingu [1] ndiyo antifona pekee inayotumika kumalizia Sala ya mwisho ya Liturujia ya Vipindi [2] lakini pia inashika nafasi ya sala ya Malaika wa Bwana (inayotumika karibu mwaka mzima mara tatu kwa siku: asubuhi, adhuhuri na jioni).
Uenezi wa sala hiyo umechangia kiasi chake kufanya wasanii wajitokeze kumchora au kuchonga sanamu ya Maria akiwa anatawazwa au ameshatawazwa kama malkia.