Umwilisho • Utoto wa Yesu • Ubatizo Arusi ya Kana • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu • Miujiza ya Yesu Kugeuka sura • Karamu ya mwisho • Msalaba wa Yesu • Maneno saba Kifo cha Yesu • Ufufuko wa YesuKupaa mbinguni • Ujio wa piliInjili • Majina ya Yesu katika Agano Jipya • Yesu kadiri ya historia • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia
Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Ndugu wa Yesu • Yohane Mbatizaji
Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa
Mtoto Yesu kupatikana hekaluni ni tukio la maisha ya Yesu lililosimuliwa na Mwinjili Luka katika Injili yake, 2:41-52.
Ni tukio pekee la namna hiyo katika Agano Jipya lote[1] na linaripoti maneno ya kwanza ya Yesu yanayojulikana. Humo anaonyesha kujitambua kama Mwana wa Mungu, si mtoto wa Yosefu[2]
Tukio hilo limekuwa fumbo la tano katika ya yale ya furaha ya Rozari.[1]
Pia limechorwa mara nyingi na wasanii Wakristo hadi karne ya 19.
Lk 2:41 Basi, wazee wake huenda Yerusalemu kila mwaka, wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Na alipopata umri wake miaka kumi na miwili, walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuu; 43 na walipokwisha kuzitimiza siku, wakati wa kurudi kwao, yule mtoto Yesu alibaki nyuma huko Yerusalemu, na wazee wake walikuwa hawana habari. 44 Nao wakadhani ya kuwa yumo katika msafara; wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao; 45 na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta. 46 Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake. 48 Na walipomwona walishangaa, na mama yake akamwambia, Mwanangu, mbona umetutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni. 49 Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu? 50 Nao hawakuelewa na neno hilo alilowaambia. 51 Akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake.
52 Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.