Wanaotumia neno hilo wanamaanisha kuwa Maria alishiriki kwa namna ya pekee[5][6] kazi ya ukombozi iliyofanywa na Mwanae, Yesu Kristo, Mwokozi pekee[7], kwa kuwa Maria pia alikombolewa naye, isipokuwa alikombolewa vizuri kuliko wengine wote.
Ni kwamba Maria alitupatia kielelezo cha kuungana na mateso ya Mwana na kutoa fidia kwa ajili yetu. Alikubali kifodini cha Mwanae mpenzi ambaye alimuabudu kwa haki na kumpenda kwa hisani isiyosemeka. Shujaa kuliko Abrahamu aliyekuwa tayari kumchinja Isaka, Maria alipomtoa Mwanae kwa wokovu wetu alimuona akifa kwa mateso ya kutisha ya mwili na roho. Hakuna malaika aliyeingia kati kuisimamisha sadaka ya Maria na kumuambia, “Sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee” (Mwa 22:12). Maria aliona ilivyotimia sadaka ya Yesu, ambayo sadaka ya Isaka ilikuwa kidokezo chake tu, akateseka kwa ajili ya dhambi kadiri ya upendo wake kwa Mungu anayechukizwa nazo, kwa Mwanae aliyesulubiwa nazo, na kwa roho zetu zinazoangamizwa nazo. Kwa kuwa upendo wa Bikira ulizidi ule wa Abrahamu, maneno aliyoambiwa babu huyo yanamfaa zaidi Mama wa Kanisa: “Kwa kuwa umetenda neno hili… katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni” (Mwa 22:16-17).
↑“Therefore, one can say, she [that is, the Blessed Virgin] redeemed with Christ the human race.” Pope Benedict XV, Apostolic LetterInter soldalica, AAS 1918, 181.
↑St. Ambrose, De inst. virg. 7, cited from Ott, Dogmatics.
Marejeo
Ludwig Ott, Fundamentals of Catholic Dogma, Mercier Press Ltd., Cork, Ireland, 1955.