Umwilisho • Utoto wa Yesu • Ubatizo Arusi ya Kana • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu • Miujiza ya Yesu Kugeuka sura • Karamu ya mwisho • Msalaba wa Yesu • Maneno saba Kifo cha Yesu • Ufufuko wa YesuKupaa mbinguni • Ujio wa piliInjili • Majina ya Yesu katika Agano Jipya • Yesu kadiri ya historia • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia
Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Ndugu wa Yesu • Yohane Mbatizaji
Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa
Yesu kuzaliwa na Bikira ni fundisho la imani linalosema kuwa Yesu Kristo alitungwa tumboni mwa mama yake, Bikira Maria, kwa uwezo wa Mungu (Roho Mtakatifu) tu, na kuwa Maria alipomzaa alikuwa bado bikira.
Katika Biblia ya Kikristo fundisho hilo linapatikana katika Injili mbili zilizo tofauti hata kwa vyanzo katika uzazi na utoto wa Yesu: Math 1:18-25[1] na Lk 1:26-38[2].
Mathayo anathibitisha hilo kwa kutaja utabiri wa maneno ya Isa 7:14 katika tafsiri ya Kigiriki ya Septuaginta: "Tazama bikira atachukua mimba, naye atazaa mwana, nao watamwita jina lake Emmanuel, yaani Mungu pamoja nasi".[3] [4]
Fundisho hilo linashikiliwa na madhehebu karibu yote ya Ukristo, hasa Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki.
Hata Waislamu wanakubali fundisho hilo kutokana na Kurani, hasa sura 3 (Al Imran) na 19 (Maryam (sura)).[5]
Mara nyingine fundisho hilo linachanganywa na mengine tofauti,[6] kama vile utakatifu usio na doa wa Maria[7][8]na ubikira wa kudumu aliokuwa nao maisha yake yote[9]
{{cite book}}