Ulinzi wa Mama wa Mungu (kwa Kigiriki Σκέπη, Sképē; kwa Kislavi cha Kikanisa Покровъ, Pokrov, yaani "ulinzi") ni sikukuu ya Bikira Maria inayoadhimishwa na Waorthodoksi na Wakatoliki wa Mashariki wanaofuata mapokeo ya Kigiriki.
Inatokana na imani ya Wakristo wengi katika uwezo wa sala ya Mama wa Mungu kwa ajili ya binadamu.
Tarehe ya sikukuu hiyo ni 14 Oktoba (1 Oktoba kadiri ya kalenda ya Juliasi).