"I Just Can't Stop Loving You" ni jina la kutaja wimbo wa ballad ulioimbwa na Michael Jackson akimshirikisha Siedah Garrett. Wimbo huu umetungwa na Jackson, kiasili ulinuiwa uimbwe pamoja na wanawake vipenzi wa Jackson: aidha Barbra Streisand au Whitney Houston. Hata Aretha Franklin na Agnetha Fältskog (mwanachama wa zamani wa kundi la ABBA) waimbe kwenye wimbo huu, lakini waimbaji wanne hao wote walikuwa na majukumu mengine.
Hata hivyo, mtunzi na Quincy Jones wakampendekeza Garrett, ambaye ndiye aliyeandika ukumbusho wa Jackson "Man in the Mirror", amejitolea kuimba na Jackson hivyo kupelekea Garrett kuwa kwa mara ya kwanza kushiriki kwenye kibao kikali tangu kibao cha 1984 cha Dennis Edwards, "Don't Look Any Further".