"Give In to Me" ni jina la kutaja wimbo wa kumi wa mwanamuziki Michael Jackson kutoka katika albamu yake ya mwaka wa 1991, Dangerous. Wimbo huu ulishika nafasi ya #1 nchini New Zealand kwa majuma manne, na namba #2 kwenye chati za UK Singles Chart. Wimbo huu haujatolewa kule Amerika ya Kaskazini wala huko Asia.
Muziki wa Video
Muziki wa video wa "Give In to Me" unamwonyesha Michael Jackson akiimba kwenye ukumbi na moja ya wanachama wa zamani wa bendi ya Guns N' Roses. Wanachama hao ni pamoja na Slash, Gilby Clarke na mpigaji kinanda wa Guns N' Roses Teddy Andreadis wakiwa ndani ya konseti la ndani la rock. Kwa mujibu wa Jackson mwenyewe - pale alipohojiwa na Oprah - ilikuwa imetoka kupigwa video yake masaa mawili nyuma kule nchini Ujerumani. Ile mimwanga-mwanga inayoonekana kwa nyuma kwenye video ni maujanja ya kompyuta tu na yamekuja kuwekwa hapo baadaye.
Chati
Orodha ya Nyimbo
- "Give In to Me" – 5:26
- "Dirty Diana" – 4:52
- "Beat It" – 4:17
Marejeo
Viungo vya Nje
|
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Give In to Me kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|