Mlima

Mlima Kilimanjaro unavyoonekana kutoka Moshi
Mlima Denali jimboni Alaska (USA).

Mlima ni sehemu ya uso wa dunia iliyoinuka sana juu ya mazingira yake.

Mifano katika Afrika ni Mlima Kilimanjaro na Mlima Kenya.

Kilele na vilele

Kwa kawaida mlima huwa na kilele kimoja au zaidi; kwa mfano Kilimanjaro huwa na vilele vitatu vya Kibo, Mawenzi na Shira. Kama mlima ni mpana sana vilele vyake vinaweza kuitwa mlima kila mmoja; kama mwinuko fulani hutazamwa kama mlima wa pekee au kama kilele kimojawapo hutegemea uzoefu. Wakati mwingine Kibo hutajwa kama "mlima" si kama kilele cha Kilimanjaro pekee, halafu kwa maana huu Kilimanjaro si mlima mmoja bali safu ndogo ya milima.

Milima mikubwa, milima midogo

Kama mlima unatazamwa kama mrefu au la hutegemea mazingira yake. Katika nchi tambarare kabisa hata miinuko midogo ya mita 100 inaweza kuitwa "mlima". Katika eneo lenye milima mingi na mirefu mwinuko wa mita 1000 mara nyingi hukubaliwa kama mlima kwa sabau ni mdogo kulingana na milima mikubwa.

Lugha nyingi zinatofautisha kati ya milima mikubwa na midogo au vilima, kwa mfano Kiingereza kwa maneno kama "mountain" na "hill". Lakini hata hapa hutegemea mazingira kama sehemu fulani huitwa hill au mountain. Uingereza huwa na sheria inayoita kila sehemu juu ya mita 600 "mlima".

Urefu wa mlima hutajwa kitaalamu kwa "mita juu ya uwiano wa bahari". Hata hivyo mlima unaweza kuonekana mdogo kiasi kama mazingira yake ni nyanda za juu na mwinuko wake juu ya nyanda za juu si mrefu sana; kinyume chake hata mlima mdogo kiasi unaweza kuonekana mkubwa kabisa kama mazingira yake ni yote tambarare karibu na uwiano wa bahari.

Milima na maisha

Milima huwa muhimu kwa ekolojia ya uhai na maisha ya binadamu kwa sababu milima ni mahali pa mvua nyingi kushinda mazingira. Mito mingi duniani inaanza milimani na hupeleka maji kutoka huko kwenda tambarare na mabonde.

Kutokea na kupotea kwa milima

Milima huwa na historia inayoweza kutazamwa kama maisha ya mlima. Milima hutokea kutokana na miendo ndani ya ganda la dunia.

Mabamba ya gandunia husukumana na kusababisha shinikizo linalosababisha ufa mkubwa kwa sehemu fulani. Baada ya kuvunjwa kwa sehemu kubwa ya mwamba mwendo wa ganda la dunia unaweza kusukuma kipande kimoja juu.

Milima kunjamano kama Himalaya katika Asia, Alpi ya Ulaya au Atlas ya Afrika ya Kaskazini ilitokea pale ambapo mabamba mawili ya gandunia yalikutana na kugongana.

Miendo ya gandunia husababisha pia kutokea kwa milima baharini inayoweza kutokeza juu ya uso wa maji kama visiwa. Milima iliyotokea kutokana na kukunjwa mara nyingi huonekana kama safu ndefu ya milima.

Njia nyingine ya kutokea kwa milima ni volkeno. Hapo magma (mwamba moto ulioyeyuka) inapanda kutoka koti ya dunia inakuta njia kupitia nafasi katika ganda la dunia na kufika usoni kwa umbo la zaha (lava). Hapa zaha inaganda kuwa mwamba imara. Kama akiba ya magma chini ya volkeno ni kubwa inaendelea kupanda juu na kutoka kwenye kasoko za volkeno. Inapanda juu ya zaha iliyoganda tayari na kwa njia hii volkeno inazidi kukua. Volkeno kubwa Afrika ni Kilimanjaro.

Baada ya kutokea milima inaendelea kupungua polepole kutokana na miamba kuvunjika na kusagwa kwa njia ya mmomonyoko. Athari zinazosababisha mmomonyoko ni hasa tofauti za halijoto pamoja na maji, upepo na barafu. Wakati wa joto mwamba hupanuka kiasi, wakati wa baridi hujikaza na kwa njia hii hutokea ufa ndani yake. Hapo maji yanaweza kuingia na kuganda kuwa barafu wakati wa baridi yakizidi kupanua ufa na kuvunja mwamba polepole.

Milima mirefu duniani

tazama makala kuu: Orodha ya milima mirefu duniani

Mlima mrefu unaojulikana kabisa uko nje ya dunia kwenye sayari Mirihi: unaitwa Olympus Mons na kuwa na urefu wa kilomita 27.

Mlima mrefu juu ya uso wa dunia huitwa Mount Everest (mita 8,848) uko mpakani mwa nchi ya Nepal na Tibet (China) katika Asia.

Lakini mlima mrefu kabisa ni Mauna Kea katika funguvisiwa la Hawaii. Unaonekana kama mlima mrefu wa Hawaii unaofikia mita 4,214 juu ya UB, lakini ukitazamwa kutoka chanzo chake unapoanza kuinuliwa juu ya mazingira yake chini ya bahari kilele chake kipo mita 10,205 mita juu ya mazingira tambarare yaliyoko chini ya bahari.

Milima mirefu ya kila bara ni kama ifuatavyo:

Vilele vilivyo mbali zaidi na kiini cha Dunia

Mlima Everest ndio mlima mrefu zaidi duniani, lakini si wenye kilele cha mbali zaidi kutoka katikati mwa dunia, kwa sababu ya kujikunja kwa Ikweta.

Nafasi Mlima Kimo juu ya
kitovu cha Dunia
kwa mita
Mita juu ya
usawa wa bahari
Nchi
1. Chimborazo 6,384.557 &0000000000006267.0000006,267 Ekwador
2. Huascaran 6,384.552 &0000000000006768.0000006,768 Peru
3. Cotopaxi 6,384.190 &0000000000005897.0000005,897 Ekwador
4. Kilimanjaro 6,384.134 &0000000000005895.0000005,895 Tanzania
5. Cayambe 6,384.094 &0000000000005796.0000005,796 Ekwador
6. Mount Everest 6,382.414 &0000000000008848.0000008,848 Nepal

Picha

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!