Australia na Visiwa vya Pasifiki (pia: Oceania, Okeania, Oshania) hujumlishwa mara nyingi pamoja katika hesabu ya mabara.
Hasa watu kwenye visiwa vingi vya Pasifiki wana utamaduni wa karibu. Vilevile historia ya visiwa hivyo kabla ya kuenea kwa ukoloni imefanana katika mengi.
Kwa lugha nyingi za dunia jina la "Oceania" (Okeania, Oshania) limekuwa la kawaida kutokana na neno la Kigiriki "okeanos" (kwa Kilatini: oceanus; kwa Kiingereza: ocean). Hivyo "Oceania" yamaanisha "nchi katika bahari". Ila tu hatuoni faida ya kuingiza neno hili katika lugha ya Kiswahili kwa sababu ni neno lisiloeleweka vizuri. Mara wataalamu hujadili "Oceania" kuwa visiwa vya Pasifiki pamoja na Australia; mara wanaona "Oceania" ni visiwa vile pekee bila Australia na wengine wanasema wenyewe "visiwa vya Pasifiki" ingekuwa jina zuri zaidi kama Australia haihesabiwi.
"Australasia" imekuwa jaribio tofauti la kutaja eneo, hasa kati ya wataalamu wa Australia, ila tu halipendwi na watu wengi visiwani. Hivyo imetumiwa zaidi kwa kanda la Australia na visiwa jirani pekee.
Eneo
Visiwa vyote kwa pamoja (bila Australia yenyewe) hukadiriwa kuwa 7,500 vyenye eneo la nchi kavu la kilomita za mrabamilioni 1.3 vilivyosambaa katika eneo la bahari la kilomita za mraba milioni 70. Takriban visiwa 2,100 vimekaliwa na watu milioni 14.9.
Visiwa vingi katika Pasifiki ni milima ya volkeno inayoinuka kutoka tako la bahari hadi uso wa maji; mara nyingi zinaonyesha kasoko. Visiwa vingine vinajengwa na matumbawe yanayokua juu ya volkeno ambazo zimeishia kidogo chini ya uso wa bahari. Visiwa vingine ni atoli ambako matumbawe yamejenga tuta tumbawe kwa umbo la mviringo kuzunguka kisiwa cha kivolkeno.
Sababu ya kutokea kwa volkeno nyingi ni miendo ya gandunia katika tabaka za ganda la dunia chini ya bahari. Ngozi ya nje au ganda la dunia hufanywa na vipande mbamlimbali (=mabamba ya gandunia) vinavyoelea juu ya tabaka ya mwambamoto na kiowevu. Pale ambako vipande hivi vinagusana mara kwa joto na mwamba moto ulioyeyuka unapanda juu; pale ambao kupanda huku kunatokea haraka tunaona volkeno na hivyo kisiwa kipya kutokea. Mfano ni safu ya visiwa vya Hawaii ambavyo ni safu ya milima ya volkeno inayoanza kwenye tako la bahari, mengine inaonekana kama visiwa, mengine iko chini ya uso wa bahari.
↑Tokelau ni eneo la New Zealand na haina makao makuu kwa jumla kila kisiwa kina chake.
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!