Tabaka la viongozi wa kisiasa na wa kijeshi walikuwa Waosmani waliokuwa Waturuki pamoja na mchanganyiko wa Waislamu kutoka sehemu zote za milki yao, hasa Balkani. Kwenye uwanja wa uchumi na utawala Waosmani walitumia sana Wakristo Wagiriki na Waarmenia kutokana na elimu yao.
Milki ilianza kama eneo dogo la kabila la Kituruki katika Anatolia chini ya chifuOsmani I likaendelea kupanuka hasa kwa kutwaa sehemu za milki ya Bizanti upande wa Asia na Ulaya ya Kusini-Mashariki.
Mwaka 1453 Waosmani walitwaa mji wa Konstantinopoli na kumaliza Milki ya Bizanti wakifanya mji kuwa mji mkuu wao.
Kilele cha enzi yake ilikuwa katika karne ya 16 hadi 17. Mwaka 1683 Waosmani walijaribu mara ya pili kuvamia Austria na kuteka Vienna lakini walishindwa. Kuanzia tukio hilo athira yao katika Ulaya ilianza kupungua.
Wakati wa karne ya 19 Milki ya Osmani ikaitwa "Mzee mgonjwa wa Ulaya" (pia: "Mgonjwa wa Bosporus") na ilikuwa hasa mashindano kati ya Urusi, Ufaransa, Uingereza na Austria-Hungaria yaliyozuia kushindwa kwake kwa sababu kila nchi kubwa ya Ulaya ilihofia ya kwamba nchi nyingine ingejipatia sehemu kubwa za Milki ya Osmani, hivyo walizuiliana. Lakini nguvu yake iliendelea kufifia.
Kwenye mwisho wa karne ya 19 Masultani walijaribu kutekeleza matengenezo mbalimbali ya muundo wa kisiasa na kiuchumi lakini mabadiliko yalitokea polepole.
Mwisho wa milki ilikuja katika vita viwili vya mwanzoni wa karne ya 20.
Vita vya Balkani viliondoa karibu nchi zote upande wa Ulaya kutoka utawala wa Waosmani.
Mwaka 1918 jeshi na dola vikaporomoka kabisa. Milki ikagawiwa na washindi wa vita. Sehemu za Kiarabu zikawa nchi lindwa za Uingereza na Ufaransa. Katika maeneo yaliyobaki nchi mpya ya Uturuki ikaanzishwa.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Uturuki kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!