Sekundi, Karpofori na wenzao Viktorini na Severiani (walifariki mwishoni mwa karne ya 3 au mwanzoni mwa karne ya 4) ni kati ya mashahidi wa imani ya Kikristo waliouawa huko Albano, karibu na Roma (Italia) wakati wa dhuluma ya Dola la Roma[1].
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kati ya watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 8 Agosti[2].