Visiwa vya jamhuri vimesambaa katika eneo pana sana:
Kisiwa kikuu cha Mauritius ni km² 1,865 au 91% za ardhi yote ya jamhuri. Karibu wakazi wote (1,261,208) huishi huko.
Kisiwa cha Rodrigues kipo km 560 mashariki kwa Morisi yenyewe. Eneo lake ni km² 109; kuna wakazi 41,000.
Visiwa vya Cargados Carajos (vinaitwa pia Saint Brandon) ni visiwa 16 vidogo sana, vyenye eneo la km² 1.3 pekee. Viko km 300 kaskazini kwa Morisi. Kuna wakazi mia chache wavuvi.
Agalega ni visiwa viwili, yaani Kisiwa cha Kaskazini na Kisiwa cha Kusini, takriban km 1,122 kaskazini kwa Morisi yenyewe. Visiwa hivyo vina eneo la km² 70. Kuna vijiji vya Vingt Cinq na La Fourche kwenye kisiwa cha kaskazini na kijiji cha Ste Rita kwenye kisiwa cha kusini. Wenyeji wanalima mazao ya mnazi pamoja na mboga kwa matumizi yao wenyewe.
Baada ya Waarabu na Wareno kuvumbua Morisi, wakazi wa kwanza (1638) walikuwa Waholanzi, lakini hawakuacha dalili isipokuwa majina ya mahali kwa sababu waliondoka mwaka 1710 baada ya kushindwa kiuchumi.
Baada ya kuwapatia watumwa uhuru, Waingereza walileta Wahindi wengi, baadaye pia Wachina kama wafanyakazi kwenye mashamba ya sukari. Leo hii idadi kubwa ya wakazi ni wa asili ya Uhindi (67%), wakifuatwa na Waafrika (28%), Wachina (3%) na Wafaransa (2%).
Nchi iliendelea kuwa na serikali zilizochaguliwa bila kupinduliwa: hali hii ya utulivu ilisaidia kukua kwa uchumi. Hali ya maisha ni ya juu kuliko nchi nyingi za Afrika.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Morisi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!