Wilaya ya Rungwe ni eneo lenye mvua nyingi katika Tanzania, ila maeneo makubwa ya Wilaya ya Chunya ni makavu.[2].
Mkoa kwa ujumla ni mmojawapo kati ya mikoa yenye kilimo kizuri inayotoa mazao ya kulisha taifa Mbeya na Mbozi kahawa hupandwa. Rungwe pana chai nyingi, pamoja na Rungwe na Chimala hulimwa mpunga. Nyanda za juu kuna nafaka na viazi.
Mbeya inahudumiwa na Kituo cha Reli cha Mbeya ambacho kiko karibu na A104 au kupitia reli ya TAZARA kutoka mjini, kwa wiki hupokea treni mbili za abiria.[4]
Barabara
Mbeya inaweza kufikiwa kwa barabara kwenye barabara kuu ya A-7 kutoka Dar es Salaam , Kuna barabara za lami ambazo zinaunganisha jiji la Mbeya na miji mingine kama Tukuyu kupitia Uyole, Tunduma kupitia barabara kuu ya TANZAM na Chunya hadi Tabora kupitia Isanga.
Mbeya ina idadi kubwa ya abiria wanaoelekea Lusaka/Malawi kutoka Bandari ya Dar es Salaam ambao mara nyingi husimama mjini kwa ajili ya malazi ya usiku au chakula.
Uwanja wa Ndege
Mbeya inaunganishwa na Tanzania nzima kwa njia ya ndege kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe ambao ulifunguliwa Desemba 2012. Ni moja kati ya viwanja vinne vikubwa vya ndege vilivyopo Tanzania. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe uko ndani ya mkoa wa Mbeya na sio katika mkoa mpya wa Songwe. Uwanja huo upo umbali wa kilomita 25 kutoka katikati ya Jiji la Mbeya na umbali wa kilomita 2-3 kutoka mpaka wa mikoa ya Mbeya na Songwe ambao ni mto Songwe.
Vivutio vya kitalii
Ziwa Ngosi ni ziwa la pili kwa ukubwa barani Afrika lililotokana na mlipuko wa volkeno. Linapatikana karibu na Tukuyu, mji mdogo katika Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.
Daraja la Mungu la Kiwira
Maporomoko ya maji ya Mwalalo.
Maporomoko ya maji ya Kapologwe yapatikana Mbeya
Mbeya ni kati ya maeneo yanayopendeza kabisa ndani ya Tanzania ikiwa na sehemu za ziwa Nyasa, Mlima ya Mbeya, Mlima ya Rungwe, Uwanda wa juu wa Uporoto, Uwanda wa Usangu ingawa haukufikiwa bado na utalii.[2]
Mvua kwa kawaida huanza mwezi Oktoba na kumalizika mwezi Mei, ikifuatiwa na kipindi kikavu na baridi kati ya Juni na Septemba. Utalii wa kawaida sio mchangiaji mkubwa wa uchumi wa ndani na hakuna miezi inayoonekana kuwa na watalii wengi.
Mbeya ipo katika Bonde la Ufa na unachukuliwa kama Csb na mfumo wa Köppen-Geiger. Hali ya hewa ya baridi na milima katika mji huvutia hasa wenyeji kutoka sehemu zingine za nchi na wageni kwa ajili ya michezo na uvuvi. Serikali ya eneo hilo imeanza kujaribu kupanua utalii zaidi ya kutazama wanyama pori, na imewekeza katika kuzalisha ramani bora na kuendeleza kituo cha utalii cha ndani.[5]
Mbeya pia ina maeneo mbalimbali ya michoro ya kwenye miamba na mapangoni. Maeneo mengi ya miamba bado hayajasajiliwa na idara ya Antiequits na kutoa kioo cha kuangalia katika tamaduni za jadi za jamii zinazozunguka.
Majimbo ya bunge
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
↑"TANZAM JOURNEY | Railways Africa". web.archive.org. 2012-04-23. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-04-23. Iliwekwa mnamo 2024-08-28.{{cite web}}: CS1 maint: bot: original URL status unknown (link)
↑"Tourism and Wildlife | Mbeya Region". web.archive.org. 2016-02-08. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-02-08. Iliwekwa mnamo 2024-08-28.{{cite web}}: CS1 maint: bot: original URL status unknown (link)
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Mbeya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!