Tukuyu ilianzishwa mnamo 1901 wakati wa ukoloni wa Kijerumani. Wajerumani waliwahi kuunda kituo cha kwanza pale Lumbila ya leo, kando ya Ziwa Nyasa wakakiita "Langenburg"[1] kwa heshima ya kabaila na mwanasiasa Mjerumani. Langenburg iliendelea kuwa makao makuu ya Mkoa wa Langenburg lakini ilikuwa na matatizo machoni pa Wajerumani walioona tabianchi haifai kwao kiafya. Mwaka 1900 waliamua kuhamisha makao makuu sehemu iliyokuwa baridi zaidi na kujulikana kwa jina Tukuyu wakaiita "Neu Langenburg" ("Langenburg mpya"). Boma jipya lilijengwa mwaka 1901. Hadi leo jina la hoteli "Langiboss" linakumbusha jina la zamani. Neu Langenburg iliendelea kuwa mji mdogo; mnamo 1913 ilikuwa na maduka 10 na kituo cha polisi chenye askari 66.
Pia ni kitovu cha kilimo cha ndizi za kuiva: takribani mkoa wote wa Mbeya hutegemea ndizi kutoka Tukuyu.
Kwa miaka mingi Tukuyu ilikuwa na tatizo la mawasiliano mabaya kutokana na uharibifu wa barabara pamoja na matatizo ya kisiasa kati ya Malawi na Tanzania.
Siku hizi barabara ni nzuri kuelekea Malawi, pia kwenda Mbeya na Daressalaam.
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Tukuyu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!