Katika lugha zote za kisasa bahari inaitwa "bahari nyeusi": Kigiriki Μαύρη θάλασσα, Kibulgariacherno more (Черно море), Kigeorgiashavi zghva (შავი ზღვა), KiromaniaMarea Neagră, Kirusichyornoye more (Чёрное море), KiturukiKaradeniz, Kiukrainechorne more (Чорне море).
Jina hili limepatikana kwa hakika tangu karne ya 13 lakini asili yake haijulikani.
Wagiriki na Waroma wa Kale waliita Euxeinos Pontos (Εὔξεινος Πόντος) au "Bahari ya ukarimu".
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bahari Nyeusi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.