"2 of Amerikaz Most Wanted" ni wimbo wa hip hop uliotungwa na 2Pac, Snoop Dogg na Daz Dillinger kwa ajili ya albamu mbili za pamoja za 2Pac, All Eyez on Me. Wimbo umeimbwa na watu wawili ambao ni 2Pac na Snoop Dogg. "2 of Amerikaz Most Wanted" ulitolewa kama wimbo wa promosheni na ulitolewa kama single ya pili kutoka albamu , baada ya "California Love". Wimbo umeshika nafasi ya 46 kwenye Billboard Hot R&B/Hip-Hop Airplay.
"2 of Amerikaz Most Wanted" pia iliingizwa kwenye 2Pac's Greatest Hits mnamo 1998. Remix ya wimbo pia iliingizwa kwenye albamu ya Nu-Mixx Klazzics mnamo 2003.