Yohane Mbatizaji Garcia (Almodóvar del Campo, Ciudad Real, Hispania, 10 Julai 1561 - Cordoba, Hispania, 14 Februari 1613) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mtawa wa shirika la Watrinitari, yaani watawa wa Utatu mtakatifu, waliojitoa kabisa kwa ajili ya kukomboa Wakristo waliotekwa utumwani.
Alijitahidi kufanya urekebisho wa shirika hilo kwa kuanzisha tawi la Watrinitari Peku kwa kufuata mfano wa Teresa wa Yesu kati ya vipingamizi vikubwa na tabu nyingi [1].
Pia aliandika vitabu vingi vya teolojia.
Alitangazwa na Papa Pius VII kuwa mwenyeheri tarehe 26 Septemba 1819, halafu Papa Paulo VI alimtangaza mtakatifu tarehe 25 Mei 1975[2].
Sikukuu yake ni tarehe 14 Februari[3].
{{cite web}}