Wikipedia ya Kislovakia (Kislovakia: Slovenská Wikipédia) ni toleo la kamusi elezo ya Wikipedia kwa lugha ya Kislovakia. Ilianzishwa mnamo mwezi wa Oktoba katika mwaka wa 2003, lakini ikaanza kufanya kazi kwa sana katikati mwa mwaka wa 2004.
Ilielezwa ya kwamba Wikipedia hii ilifikisha makala 15,000 mnamo mwezi Septemba 2005 na kiwango cha makala 50,000 kilifikia kunako mwezi wa Agost 2006 na kiwango cha makala 100,000 kilifikia kunako mwezi wa Agosti 2008.
Wikipedia ya Kislovakia imefikisha makala zaidi ya 100,000 kunako tar. 28 Agosti 2008. Wikipedia ya Kislovakia ni miongoni mwa Wikipedia kubwa katika orodha ya matoleo ya Wikipedia za Lugha za Kislavoni. Kuna kiasi kikubwa sana cha maboti yanayoanzisha makala katika Wikipedia ya Kislovakia.