Serapioni wa Aleksandria (alifariki 212 hivi) alikuwa Mkristo wa Misri aliyechomwa moto kwa ajili ya imani yake kwa amri ya gavana Akwila wakati wa dhuluma ya kaisari Septimius Severus[1].
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 13 Julai[2][3].
Mwingine mwenye jina hilohilo (alifariki 248 hivi) alikuwa Mkristo wa Misri aliyeteswa vikali sana kwa kuvunjwa viungo vyote vya mwili kabla ya kurushwa kutoka ghorofani kwa ajili ya imani yake wakati wa dhuluma ya kaisari Decius[4].
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 20 Februari[5][6] au 14 Novemba[7].
Mwingine tena mwenye jina hilo alifia Ukristo kwa kutoswa baharini pamoja na Kronide na Leonsi ndugu yake wakati wa dhuluma ya kaisari Maximian (mwishoni mwa karne ya 3).
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 12 Septemba[8][9].