Kronide, Leonsi na Serapioni (walifariki mwishoni mwa karne ya 3 au mwanzoni mwa karne ya 4) walikuwa Wakristo wa Misri waliotoswa baharini kwa ajili ya imani yao wakati wa dhuluma ya kaisari Maximian[1].
Wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama watakatifu wafiadini, pengine pamoja na Seleusi, Stratoni na Valeriani [2]
Sikukuu yao inaadhimishwa kila mwaka tarehe 12 Septemba[3].