Kijani - Njano - Nyekundu kwa kufuata mfano wa Ethiopia
Rangi tatu za kijani, njano na nyekundu huitwa rangi za umoja wa Afrika kwa sababu zinapatikana kwenye bendera ya Ethiopia, nchi pekee ya Afrika iliyofaulu kujitetea dhidi ya uvamizi wa kikoloni katika karne ya 19BK.
Tangu kuenea kwa uhuru kwenye nchi za Afrika katika miaka ya 1950 na 1960 kuna nchi mbalimbali zilizochagua rangi zilezile kwa kuonyesha upendeleo wao kwa umoja wa Afrika. Ghana ilikuwa nchi ya kwanza ya kutoka katika ukoloni mwaka 1957 ikateua rangi za Ethiopia kwa bendera yake.
Bendera za nchi zifuatazo hutumia rangi za Ethiopia ama pekee au pamoja na rangi nyingine, ambayo mara nyingi ni nyeusi kama alama ya watu weusi.
Bendera za nchi kadhaa za Amerika zinatumia rangi zilezile kwa sababu wakazi wao ni watoto wa watumwa kutoka Afrika.
Nyekundu - Nyeusi - Kijani kwa kufuata mapokeo ya Marcus Garvey
Kuna seti nyingine ya rangi iliyoundwa kwa nia hiyohiyo lakini asili yake iko zaidi Amerika ambako imekuwa bendera ya watu wanaopigania haki za watu weusi ambao ni wajukuu wa watumwa wa zamani na umoja nao na Afrika. Hii bendera inatumia ranginyekundu, nyeusi na kijani.
Hii ilikuwa bendera ua UNIA (Universal Negro Improvement Association and African Communities League) nchini Marekani. Ilipendekezwa na Marcus Garvey aliyeeleza mwaka 1921 "nyekundu ionyeshe urafiki na "wekundu kote duniani" (Wasoshalisti waliotumia bendera nyekundu walikuwa chama cha kupinga ubaguzi wa rangi), kijani ionyeshe urafiki wa watu wa Eire (wakati ule Waeire (wa Ireland) walipigania uhuru kutoka Uingereza wakitumia bendera ya kijani) na nyeusi kwa watu weusi"[1].