Bendera ya Ethiopia mara nyingi inatajwa kuwa bendera ya kwanza ya kiafrika. Rangi zake ni kijani kibichi, njano na nyekundu. Kutokana na sifa za Ethiopia za kuwa nchi ya pekee katika Afrika iliyojitetea dhidi ya uvamizi wa ukoloni. Rangi zake zilikuwa kama alama ya umoja na uhuru wa Afrika zikatumika kama rangi za Umoja wa Afrika katika bendera za nchi nyingi za Kiafrika.
Bendera ya rangi tatu ilitumika Ethiopia tangu karne ya 19 BK. Wakati wa serikali ya kifalme ilikuwa na nembo ya simba ya Yuda. Serikali ya mapinduzi ya DERG ilifuta simba na kubadilishabadilisha nembo za katikati. Tangu 1996 bendera imekuwa na nyota ya pembetatu.
Kama sifa hiyo ya kuwa bendera ya kwanza ya kiafrika ni kweli inategemea na namna ya kuangalia Afrika. Kwenye Afrika ya kijiografia jinsi inavyotajwa leo dola za Afrika ya Kaskazini ziliwahi bila shaka kutumia bendera tangu karne nyingi yaani muda mrefu kabla ya karne ya 19.
Nchi za Afrika zinazotumia rangi tatu za Ethiopia ndani ya bendera zao
Nchi zenye bendera ya milia mlalo (kuanzia mlia wa juu)