Bendera ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ina milia minne ya kulala ya rangi buluu - nyeupe - kijani - njano inayokatwa na mlia mmoja mwekundu wa kusimama. Ndani ya mlia wa juu kuna nyota ya pembetano njano.
Bendera hii imetungwa na Barthélemy Boganda aliyekuwa rais wa kwanza wa eneo la kujitawala wa Ubangui-Shari wakati wa mwisho wa ukoloni wa Ufaransa.
Boganda aliamini ya kwamba "Afrika na Ufaransa wanapaswa kwenda sambamba". Hivyo aliunganisha rangi za bendera ya Ufaransa (nyekundu-nyeupe-buluu) na rangi za Umoja wa Afrika (nyekundu - kijani - njano).