Albamu yake ya pili, yenye mauzo ya platinamuFear of Flying, ilitolewa mnamo 2000 na kupata mafanikio kadha wa kadha nchini Marekani na pande zingine za dunia, kwa single ya "Case of the Ex" ikawa kibao kikali na kilichovuma zaidi cha Mýa, kwa kufikia nafasi ya kwanza kwenye Australian Singles Chart. Baada ya mwaka, Harrison amejishindia tuzo yake ya kwanza ya Grammy Award kwa kibao kikali cha "Lady Marmalade", toleo la marudio ambalo amefanya na Christina Aguilera, Lil' Kim, na Pink kwa ajili ya kibwagizo cha filamu ya Moulin Rouge! (2001).
Albamu yake ya tatu, Moodring, ilitolewa mnamo mwezi wa Julai 2003 nchini Marekani na kutunukiwa Dhahabu na RIAA. Kwa kufuatia kubadili-badili studio kadhaa, ilipelekea kuchelewesha kutolewa kwa albamu ya nne ya Mýa, Liberation (2007), ilitolewa kwa mtindo wa upakuzi kupitia intaneti huko nchini Japani pekee na kumfanya atoe 2008 Japan-albamu babkuwa ya Sugar & Spice.
Kuongoza ujuzi wake katika uigizaji na kazi za uungaji mkono bidhaa, Harrison ameweza kujiingiza kwenye utangazaji wa mabishara na makapuni kama vile Coca-Cola, Gap, Iceberg, Tommy Hilfiger, na Motorola na amepta kuwa na uhusika mfupi kwenye filamu kama vile Dirty Dancing: Havana Nights (2004), Shall We Dance? (2004), na Cursed (2005). Mnamo mwaka wa 2002, amecheza kwenye filamu ya Chicago ambayo ni tengenezo la pili la filamu ya mwaka wa 1975 ya Broadway-muziki Chicago, ambayo amejishindia tuzo la Screen Actors Guild Award.[2]
Harrison alikuwa mshiriki kwenue msimu wa tisa wa Dancing with the Stars.[3]Billboard wamempa Mýa nafasi ya 97 katika orodha Wasanii Hot 100 wa miaka ya 2000.[4]