Missy Elliott

Missy Elliott
Missy Elliott mnamo mwaka wa 2010
Missy Elliott mnamo mwaka wa 2010
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Melissa Arnette Elliott
Pia anajulikana kama Missy "Misdemeanor" Elliott
Amezaliwa 1 Julai 1971 (1971-07-01) (umri 53)
Portsmouth, Virginia, United States
Aina ya muziki Hip hop, R&B, hip hop soul, club music, dance,
Kazi yake Rapper, mtunzi wa nyimbo, mwimbaji, mtayarishaji wa rekodi, mwigizaji, mnenguaji, mbunifu
Ala Masauti
Miaka ya kazi 1993–mpaka sasa
Studio The Goldmind, East West, Elektra, Atlantic, Violator
Ame/Wameshirikiana na Swing Mob, Timbaland, Nelly, Aaliyah, Ginuwine, Jodeci, Eve, Ciara, TLC, Total, Jennifer Hudson, Fantasia, Nicole Wray, Pussycat Dolls, Nelly Furtado, Paula Cole, Jazmine Sullivan, 702, Blaque, Adina Howard, Busta Rhymes, Keshia Chante, Ruslana, T-Pain, Janet Jackson, Tweet, Mariah Carey, Keyshia Cole
Tovuti missy-elliott.com


Melissa Arnette Elliott (amezaliwa tar. 1 Julai 1971) ni msanii wa rekodi, mtayarishaji, mwigizaji na mwanachama wa zamani wa bendi ya Sista kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Missy "Misdemeanor" Elliott. Akiwa na mauzo ya zaidi ya milioni saba kwa Marekani pekee,[1] ni rapa wa kike pekee kuwa na albamu sita zilizotunukiwa platinamu na RIAA,[2] ikiwa pamoja na moja kuwa na platinamu maradufu, Under Construction. Mpaka sasa, rapa huyu ameuza zaidi ya rekodi milioni 16 kwa hesabu ya dunia nzima.

Elliott anafahamika kwa mfululizo wake wa vibao vikali na video mbalimbali za muziki ikiwa ni pamoja na "The Rain (Supa Dupa Fly)", "Hot Boyz", "Get Ur Freak On", "One Minute Man", "Work It", "Gossip Folks", "Pass That Dutch", "Lose Control" na "Ching-a-Ling". Kwa namna moja au nyingine, Elliott amefanya kirefu akiwa kama mtunzi wa nyimbo na mtayarishaji kwa wasanii wengine, vyote akiwa peke yake na mtayarishaji wake na rafiki wa utotoni mwaka - Timbaland. Kazi za utunzi na utayarishaji za Elliott kwa wasanii kadhaa wengine ambao wakubwa ni pamoja na Aaliyah, Mya, Lil' Kim, Danity Kane, Mariah Carey, Keyshia Cole, Lil' Mo, Christina Aguilera, Tamia, Mary J. Blige, SWV, Beyoncé, Nelly, Ciara, TLC, Total, Jennifer Hudson, Fantasia, Nicole Wray, Pussycat Dolls, Nelly Furtado, Paula Cole, Jazmine Sullivan, 702, Blaque, Adina Howard, LeToya, Busta Rhymes, Ruslana, T-Pain, Janet Jackson, Tweet, Eve, Da Brat, Fabolous, Ginuwine, ODB, Kanye West, Static Major, Lil Wayne, Ghostface Killah, Nas, Jay-Z, Eminem, 50 Cent, Trina, Ms. Jade, Lady Luck, Omarion, Justin Timberlake, Angie Stone, Magoo, Monica, Faith Evans, Kelly Price, MC Lyte, Madonna, Brandy, Melanie Brown, Blu Cantrell, Notorious B.I.G., Diddy na Timbaland.

Maisha ya awali na kazi

Maisha ya awali

Diskografia

Albamu

Ziara
Albamu za Kompilesheni
DVD
  • Hits of Miss E… The Videos Vol.1 (2001)
  • Recipe of Hits: Music Video Anthology (2005)

Filmografia

Televisheni

Mwaka Jina Uhusika Kipengele
1997 Family Matters K.m jina lale "Original Gangster Dawg" (msimu wa 9, kipengele cha 203)
1998 The Wayans Bros. K.m jina lale
2005 MTV Cribs K.m jina lale
2005 The Road to Stardom K.m jina lale
2008 Ego trip's Miss Rap Supreme K.m jina lale Msimu wa 1
America's Best Dance Crew K.m jina lale, Guest Judge "Missy Elliott "Shake Ya Pom Pom" Challenge" (msimu wa 2, kipengele cha 7)

Filamu

Mwaka Filamu Uhusika
2001 Pootie Tang Diva
2003 Honey K.m jina lale
2004 Fade to Black K.m jina lale
Shark Tale Uncredited voice
2005 Just for Kicks K.m jina lale

Tanbihi

  1. Watson, Margeaux. "Rhymes and Reasons". Entertainment Weekly. Time Inc. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-03-27. Iliwekwa mnamo 2008-11-21.
  2. RIAA - Gold & Platinum search

Marejeo

Viungo vya Nje

Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!