Interscope Records ni studio ya muziki ya Kimarekani, inayomilikiwa na studio ya Universal Music Group, na inafanyakazi kama moja kati ya studio tatu za UMG - Interscope-Geffen-A&M. Studio ilianzishwa mnamo mwaka wa 1990.
Historia
Hapo awali
Interscope ilianzishwa mnamo mwaka wa 1990 na Bw. Jimmy Iovine, Ted Field, na Tom Whalley kwa msaada wa kifedha uliotolewa na studio ya Atlantic Records (ambayo ilikuwa inachukua asilimia 50 ya mapato ya studio).
Wakati studio inaanza kazi zake, mwanzoni zilikuwa zikisambazwa na Atlantic Records ikiwa chini ya East West Records ya Amerika.
Studio kwa mara ya kwanza ilitoa kazi ya rapa wa Kilatini-Gerardo, ambaye alishinda tano bora, kwa kibao chake mahili cha "Rico Suave" kunako mwaka wa 1991.
Mafanikio mengine ya awali na baadaye, ni pale walipotoa albamu ya kwanza ya Marky Mark and the Funky Bunch, ambayo ilikwenda moja kwa moja katika platinam za mwanzoni mwa mwaka wa 1992. Wakati wa kipindi hicho, Interscope pia ikaingia mkataba na baadhi ya wasanii wa rap na hip hop kama vile Tupac Shakur, Primus, No Doubt na Nine Inch Nails."[1]
Wasanii wa Interscope
Studio ambazo ziko chini ya Interscope
Tazama pia
Marejeo
Viungo vya nje
|
---|
|
Albamu kamili | |
---|
Albamu za kompilesheni | |
---|
Vibao vya lugha ya Kihispania | |
---|
Vibao vya lugha ya Kiingereza | |
---|
Nyimbo zingine | |
---|
Makala zinazohusiana | |
---|
|