Lil Kim
|
|
Maelezo ya awali
|
Jina la kuzaliwa
|
Kimberly Denise Jones
|
Amezaliwa
|
11 Julai 1974, mji wa New York
|
Asili yake
|
Mmarekani
|
Kazi yake
|
Msanii wa rap
|
Kimberly Denise Jones (ajulikanaye kama Lil Kim; alizaliwa katika mji wa New York, mnamo Julai 1974[1]) ni msanii wa rap wa Marekani.
Utoto
Wazazi wake, Linwood Jones na Ruby Mae[1] walitalakiana; hivyo, Kimberly aliishi na baba yake.[2] Wakati yeye alipoishi na baba yake, yeye alikuwa mwasi kwa sababu baba yake alikuwa mwanaume mkali.[2] Kwa hivyo, baba yake na yeye walikuwa na migogoro mingi.[2] Kimberly alichagua kuondoka baba yake; kwa hivyo, yeye aliishi na marafiki zake na wapenzi wake ambao waliuza dawa za kulevya.[2] Yeye alitaka kuendeleza maisha yake; kwa hivyo, yeye alichagua kufanya muziki wa rap popote maeneo ya Brooklyn na mji wa New York.[3] Yeye alikuwa na matamasha ambapo yeye alikutana msanii mwingine wa rap anaitwa The Notorious B.I.G. au Biggie Smalls (jina lake halisi lilikuwa Christopher Wallace).[3]
1995-1997 mwanzo wa kazi
Baadaye, Christopher Wallace aligeuka kuwa msanii wa rap maarufu katika nchi ya Marekani.[1] Wakati yeye alipokutana Notorious B.I.G, yeye alichagua jina lake kwa rap; kwa hivyo, yeye alichagua kuitwa Lil' Kim kwa sababu yeye alikuwa mfupi wa kama 4’11.[2] Na jina hilo Notorious B.I.G lilimpa nafasi kujiunga na kikundi cha rap Junior M.A.F.I.A na Lil' Kim alikuwa na uhusiano na Notorious B.I.G.[2] Junior M.A.F.I.A ilikuwa maarufu sana katika ulimwengu wa rap.[2] Katika mwaka wa 1995 albamu ya kwanza ya Junior M.A.F.I.A ilitolewa.[2] Albamu iliitwa Conspiracy.[2] Albamu hiyo ilipata mafanikio; kwa hivyo, albamu ilimruhusu Lil' Kim kuwa msanii maarufu.[4] Kwa hivyo, yeye alifanya kazi na kikundi cha wasanii wengine kama Total na The Isley Brothers na alianza kufanya kazi albamu ya kwanza Hardcore.[4] Albamu ya Hardcore ilipata mafanikio sana.[4] Albamu ya Hardcore aligeuka kuwa namba kumi na moja katika chati ya pop na wimbo “No Time” na Puff Daddy (Sean Combs) iligeuka kuwa namba moja kwa wimbo wa rap na namba ishirini katika chati ya pop.[2] [4] Watu wengi walimpenda Lil' Kim na albamu hii kwa sababu maneno ya nyimbo zake yalikuwa machafu.[5] Kwa mfano, yeye alifanya rap kuhusu kuwalalana wanaume wengi.[5] Katika mwaka wa 1997 yeye alitaka kufanya kazi albamu yake ya pili lakini alichagua kuacha kwa sababu Notorious B.I.G aliuawa katika mji wa Los Angeles. Ingawa yeye alikuwa mtu mwenye huzuni yeye alichagua kushiriki katika nyimbo za wasanii wengine.[2][5]
1998-2010
Kwa mfano, katika mwaka wa 1998 yeye alikuwa mshiriki katika maonyesho ya muziki ya Puff Daddy (Bad Boys Tour).[2] Katika majira ya kiangazi ya mwaka wa 2000 yeye alitoa albamu ya pili yake iliyoitwa Notorious K.I.M. kutoa heshima kwa Notorious B.I.G.[1] Albamu hiyo ilikuwa namba moja katika chati ya Billboard.[2] Katika mwaka wa 2001 yeye alitengeneza wimbo na wasanii wengine kama Christina Aguilera, Pink, na Mýa unaoitwa “Lady Marmalade”.[1] Wimbo huo ulikuwa na tafsiri tofauti kutoka wimbo wa Patti Labelle katika mwaka wa 1974.[6] Wimbo “Lady Marmelade” ulikuwa na mafanikio sana; kwa hivyo, ulikuwa namba moja katika chati ya Billboard Hot 100 kwa wiki tano.[1] Katika mwaka wa 2001 Lil' Kim alikuwa na matatizo na polisi kuhusu haki ya kuwinda.[5] Pia, yeye alidanganya baraza la wazee wa mahakama; kwa hivyo, yeye alishtakiwa kwa kosa la kusema uwongo.[5] Shtaka hili lilimathiri katika mwaka wa 2005.[1] Katika mwaka wa 2003 yeye alitengeneza albamu ya tatu yake La Bella Mafia.[1] La Bella Mafia iligeuka kuwa albamu yake ya tatu ya platinamu.[4] Katika mwaka wa 2005 yeye alitiwa hatiani kwa kosa la kusema uwongo; kwa hivyo, yeye alihitaji kulipa dola za Marekani $50,000 na baadaye yeye alihukumiwa kwenda jela kwa mwaka mmoja.[1][5] Yeye alitoa albamu ya nne yake The Naked Truth kabla ya yeye alikwenda jela.[5] Yeye aliondoka jela katika mwezi wa saba wa mwaka wa 2006.[4] Katika mwaka wa 2006 kazi yake ilianza kufifia kwa sababu matatizo ya haki yake.[5] Kwa hivyo, yeye aliondoka Atlantic Records katika mwaka wa 2008 na aligeuka msanii uhuru.[5] Yeye, alikuwa mshiriki katika wimbo wa Keyshia Cole na Missy Elliot katika mwaka wa 2007, wimbo ambao iliitwa “Let it Go”.[7] Wimbo huo ulikuwa na mafanikio sana.[7] Ulikuwa namba saba katika chati ya Billboard Hot 100.[7]
2011-sasa
Katika mwaka wa 2011, yeye alikuwa na ugomvi mkubwa na Nicki Minaj kwa sababu yeye alidhani kwamba Nicki Minaj aliiga sanaa yake.[1][5][8] Kwa hivyo, Lil' Kim alitengeneza wimbo ambao uliitwa “Black Friday”.[8] Sasa, yeye si maarufu kama zamani lakini yeye ni mshiriki katika nyimbo nyingi.[4] Kwa mfano, nyimbo za wasanii wa kisasa wa rap kama The City Girls, Rich the Kid, na Rick Ross.[4]
Marejeo