Katika karne ya 17, ufalme huo uliotawaliwa na oba (ni cheo cha mfalme wake) ulienea sehemu kubwa ya Afrika ya Magharibi.
Dahomey ilianzishwa na Waaja baada ya uhamisho wao kutoka Togo kuja Benin ya leo. Jina la Dahomey linasemekana kuwa limetokana na neno la Kifon la "dan" lenye maana ya "nyoka" - dokezo la ibada ya nyoka kusini mwa nchi.
Jina la mfalme wa kwanza ni Do Aklin aliyekuwa mmoja wa wana watatu wa mfalme wa Ardra waliogawanya ufalme kati yao mnamo 1625BK. Do Aklin aliunda mji wa Abomey ukawa mji mkuu wa Dahomey.
Waaja wa Abomey walichanganyikana na wenyeji wakawa kabila jipya la Wafon au Wadahomey. Waliratibu ufalme wao kwa kuupa serikali ya mfalme mwenye nguvu, wakaunda jeshi la kudumu.
Hasa mfalme Wegbadja aliweka utaratibu kwa vizazi vilivyofuata: mfalme alikuwa mtawala mkuu, mkoani au majimboni hapana watawala wa kieneo bali watumishi wake tu.
Ardhi yote ilitazamwa kuwa mali ya mfalme mwenyewe, mafundisho yaliyohakikisha malipo ya kodi kutoka kwa wakulima waliokubali ya kwamba nchi waliyoilima ni mali ya mfalme.
Mamlaka ya mfalme yalihakikisha nguvu ya Dahomey katika mazingira yake. Jeshi la kudumu lilimpatia chombo muhimu. Ndani ya jeshi hilo kulikuwa na kikosi kimoja cha pekee ambacho kilikuwa kikosi cha wanawake.
Wegbadja na wafuasi wake walikaza pia umuhimu wa ibada za pamoja. Wafalme wenyewe na mizimu yao walipewa nafasi muhimu. Sadaka zilienda na kila nafasi, hasa sadaka kwa mizimu ya wafalme.
Katika karne tatu za historia yake Dahomey ilikuwa kati ya wafanyabiashara wakuu wa watumwa. Pwani ya Benin ya leo ilijulikana kama Pwani ya Watumwa.
Jeshi la Dahomey lilikuwa na bunduki zilizonunuliwa kwa Wazungu wakiwauzia watumwa; silaha hizo zilitumika kwa ajili ya kupiga vita dhidi ya majirani na kujipatia wafungwa waliouzwa kama watumwa. Mapato kutoka biashara hiyo yaliwezesha wafalme wa Dahomey kununua silaha mpya.
Kuanzia karne ya 18, ufalme wa Dahomey ulidhoofika mpaka Ufaransa uliweza kuuvamia mwaka wa 1892. Dahomey ikawa chini ya ukoloni wa Ufaransa kuanzia mwaka wa 1899 hadi ilipopata tena uhuru tarehe 1 Agosti1960.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Benin kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Strategi Solo vs Squad di Free Fire: Cara Menang Mudah!