Mwanamke aliyevaa kinyago kadiri ya jadi za Msumbiji.
Historia ya Msumbiji inahusu eneo la Kusini mwa Afrika ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Msumbiji .
Wakazi wa kwanza wa Msumbiji huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani .
Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi ambao walimeza wakazi wa kwanza inavyothibitishwa na DNA .
Haijulikani lini wafanyabiashara Waarabu walianza kufika ufukoni na kujenga vituo na miji yao. Lakini utamaduni wa Waswahili ulifika hadi sehemu za mwambao wa Msumbiji. Hadi leo aina ya Kiswahili inazungumzwa kwenye visiwa vya Kirimba .
Mto wa Zambezi ilitumika kama njia ya mawasiliano na biashara kati ya Ufalme wa Mwene Mtapa (Zimbabwe) na wafanyabiashara wa pwani.
Taarifa za kimaandishi zinaanza na kufika kwa Wareno . Mwaka 1498 Vasco da Gama alifika akiwa njiani kuelekea Bara Hindi .
Baadaye Msumbiji ikawa koloni la Wareno hadi mwaka 1975 vita vya ukombozi vya miaka 1964 -1974 vilipomalizika kwa ushindi .
Hata hivyo vilifuata vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka 1977 -1992 .
Nchi huru Nchi zisizokubaliwa na umma wa kimataifa Maeneo ya Afrika ya kujitawala chini ya nchi nyingine
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu . Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Msumbiji kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari .