Yusto wa Aleksandria (askofu) (alifariki 19 Juni 129) alikuwa askofu wa sita wa Aleksandria (Misri) miaka 118-129[1].
Alibatizwa na Marko Mwinjili ambaye inasemekana alimpa uongozi wa Chuo cha Kikristo cha Aleksandria.
Kwa kuwa hayajulikani mengine kuhusu historia yake, haorodheshwi tena na Martyrologium Romanum.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Juni au 19 Juni.